Posts

Showing posts from March 24, 2025

KIFUA KIKUU. UPO KAMA HAUPO.

Image
KIFUA KIKUU. UPO KAMA HAUPO. Kifua kikuu ni nini? Watanzania wengi huutambua ugonjwa wa kifua kikuu kama TB, neno ambalo ni kifupisho cha Tuberculosis. Jina la Kiswahili la ugonjwa huu ni kifua Kikuu ambao ni ugonjwa wa kuambukiza unaoathiri mapafu na kusababishwa na bakteria (waitwao Mycrobacterium tuberculosis) . Bakteria/ Vimelea vinavyosababisha ugonjwa wa kifua kikuu huishi katika mapafu na kushambulia mfumo wa upumuaji. Ugonjwa huu husambazwa kwa njia ya hewa wakati watu walioambukizwa wanapokohoa, kupiga chafya au kutema mate. Dalili zake huanza kuonekana siku chache baada ya mtu kuambukizwa, hivyo ni rahisi kueneza ugonjwa huu kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine. Kikohozi cha muda mrefu kinachoweza kuhusisha kukoha damu, Maumivu kifua, uchovu wa mwili, kupungua uzito, Homa, Kutokwa na jasho wakati wa usiku ni baadhi ya dalili za ugonjwa huu. Ikumbukwe kwamba, kuna watu wana maambukizi ya ugonjwa wa kifua kikuu lakini hawaoneshi dalili zozote, hawajaisikii kuumwa na hawaambukizi ...