Ujinga Utakufanya Uone Kila Kitu Kipo Sawa au Kila Kitu Kina Kasoro.
Kuna madhara mengi sana ya ujinga. Ujinga huathiri hata mtizamo wa mtu na jinsi ya kuchukulia mambo. Ujinga humpofua mtu kiasi cha mtu kutoona mazuri au kutoona mabaya ndani ya kitu au jambo fulani. Mtu mjinga hujikuta haoni kasoro yoyote kwenye jambo yeye anaona kila kitu kipo sawa lakini pia anaweza asione zuri kwenye kitu fulani yeye anaona kila kitu kina makosa au kina kasoro. Ni vyema kutafuta au kujua ukweli wa jambo kabla ya kukosoa, kusifia au kuhukumu. Kwa mfano kwa kutokujua kanuni za kazi na maadili ya Uandishi wa habari mtu anaweza akamwona Mwandishi wa habari anapatia sana katika kazi yake ila kiukweli kuna dosari kadha wa kadha. Mtu mwingine naye kwa kutokujua anamwona mwandishi wa habari anakosea sana japokuwa kuna vitu vingi anapatia na ili ujue anapatia au kukosea na kwa kiwango kipi ni mpaka ujue kanuni za kazi yake, maadili na miongozo. Binti mmoja kwa jina la Ashura alikwenda kuishi kwa shangazi yake huko Muheza Tanga. Basi katika kuishi na k