Ujinga Utakufanya Uone Kila Kitu Kipo Sawa au Kila Kitu Kina Kasoro.
Kuna madhara mengi sana ya ujinga. Ujinga huathiri hata mtizamo wa mtu na jinsi ya kuchukulia mambo.
Ujinga humpofua mtu kiasi cha mtu kutoona mazuri au kutoona mabaya ndani ya kitu au jambo fulani. Mtu mjinga hujikuta haoni kasoro yoyote kwenye jambo yeye anaona kila kitu kipo sawa lakini pia anaweza asione zuri kwenye kitu fulani yeye anaona kila kitu kina makosa au kina kasoro. Ni vyema kutafuta au kujua ukweli wa jambo kabla ya kukosoa, kusifia au kuhukumu.
Kwa mfano kwa kutokujua kanuni za kazi na maadili ya Uandishi wa habari mtu anaweza akamwona Mwandishi wa habari anapatia sana katika kazi yake ila kiukweli kuna dosari kadha wa kadha. Mtu mwingine naye kwa kutokujua anamwona mwandishi wa habari anakosea sana japokuwa kuna vitu vingi anapatia na ili ujue anapatia au kukosea na kwa kiwango kipi ni mpaka ujue kanuni za kazi yake, maadili na miongozo.
Binti mmoja kwa jina la Ashura alikwenda kuishi kwa shangazi yake huko Muheza Tanga. Basi katika kuishi na kuna kuonyana na kushauriana. Siku moja Shangazi akamwambia Ashura, "Ashura usipozingatia vitu muhimu kwenye maisha, utaishi maisha ya kutangatanga utakuwa kama mbwa". Hii kauli ili tamkwa kwa wema tu lakini kumbe Ashura ilimuumiza akaona katukanwa. Haijapita siku Ashura kapiga simu kwao analalamika ananyanyaswa na kutukanwa. "Mama, shangazi kasema mimi natangatanga, kaniita mimi mbwa". Basi ikawa vita vita nauli ikatumwa Ashura akarudi kwao, ikabidi kikao kifanyike. Kuipima ile kauli ikaonekana ya kawaida mno na kama angeisema Mama Ashura, Ashura asingeona tatizo ila kwa kuwa kaisema shangazi kakosea sana. Hii ni sura ya ujinga tumeivika jina la "Asili ya Binadamu" lakini kiukweli ni Ujinga.
Mfano mwingine mwepesi tu kwenye hizi nchi zetu za Kiafrika kuna watu wanaamini serikali zao zinawatimizia mahitaji yao kwa 100% na kuna watu wanaona serikali zao zinakosea kwenye kila kitu. Kiini cha vita nyingi ni ujinga wa raia wengi katika bara letu.
Unamkuta mwananchi hawezi tofautisha kauli za maendeleo na kauli za chuki yeye zote sawa kiongozi akiongea. Na mwingine yeye kauli za chuki na kauli za maendeleo zote kwake ni mbaya.
AMKA TAFUTA MAARIFA
#againstignorance
#ATM2020
Comments