Njia 10 Nyepesi za kupata Maarifa Katika Mazingira ya Tanzania
Maarifa ni taarifa iliyobeba ukweli, ufananuzi, ujuzi, uelewa wa jumla wa kitu fulani. Kuna njia mbalimbali za kutapa maarifa. Kwa mazingira yetu ya kitanzania kuna njia nyingi za kupata maarifa na zifuatazo ni njia 10 nyepesi za kutumia katika jamii zetu....
Njia 10 za kupata maarifa
●Kujisomea vitabu mbalimbali, magazeti, makala, Majarida, vitabu vya dini. Maarifa mengi yamewekwa kwenye mfumo wa maandishi.
●Kuhudhuria semina, vikao na warsha mbalimbali. Hiyo ni pamoja na ibada za dini, Kliniki za afya, maonyesho kama vile Nanenane na mikusanyiko mingine inayohusu utoaji wa elimu.
●Simulizi, maonyo, ushauri kutoka kwa wazee na watu waliotuzunguka. Dondoo za vitu na visa mbalimbali vya kweli vya maisha hupatikana katika mfumo huu. Wazee wetu kwa uzoefu wao wa maisha na upendo wao kwetu hutuelimisha na kutupa mwongozo wa njia zipi salama katika mambo mbalimbali ya maisha.
●Kutazama Video zinazoelimisha (YouTube, Dokumentari, na vipindi vya kuelimisha kwenye TV)
●Kutembelea maeneo/Sehemu mbalimbali za hapa duniani iwe mitaa,vijijini, miji na hata sehemu za kihistoria utajua watu wanaishije, tamaduni zao nk
● Kudadisi na kutafiti mambo, ndani yake utapata maarifa.Kwa kujiuliza maswali na kwa kuuliza watu maswali.
●Kufanya Jambo.
Kila binadamu ana fikra, ndoto na mipango. Waliogundua vitu hawakuishia kufikiria tu bali walijaribu kufanya. Na kadri yalivyofanya ndivyo Mawazo yao walivyozidi kuwa boreshwa. Jaribu kufanya kitu fulani utazidi kupata maarifa na ujuzi juu yake. Utajua faida zake, changamoto zake. Kwa mfano Kilimo,ufugaji, biashara kadri unavyofanya ndivyo unapata ujuzi zaidi kuliko yule asiyefanya. Wahenga wanasema "Kadri Ufanyavyo Ndivyo Ubobeavyo"
●Kutokana na makosa.
Kwa kutokuwa wakamilifu siku zote wanadamu huwa tunafanya makosa. Makosa huleta maumivu pamoja na fursa ya kujifunza. Tunajifunza vitu kutokana na makosa yetu au ya wenzetu. Fanya tathimini ya hatua zako ujue wapi ulikosea, Kwanini ulikosea? Ukubwa wa athari za kosa? Ungefanya nini ili kupunguza athari? Nini kifanyake haraka ikitokea kosa limejitokeza? Nini kifanyike ili kuzuia kosa lisijirudie? Majibu ya maswali hayo ni maarifa tosha na yanatokana na kujifunza kutoka kwenye makosa yetu. Kukosea ni kujifunza. Tujifunze lakini tusiishie kulia, kulaumu au kukata tamaa pale tufanyapo makosa
● Fungua Mdomo
Kuongea ni kujifunza pia. Usikae na vitu ndani, ongea. Sema unachojua watu wakusikie. Kubali wakikukosoa kwa kile ulichosema sio sawa au hakijajitosheleza. Sema unachofikiria ndiyo utapojua pia wengine wanafikiria nini. Wafundishe wasiojua. Kuongea pia kunaongeza uwezo wa kukumbuka kile ulichoongea.
●Njia Rasmi kwa kupitia taasis za kutoa elimu
Taasis zinazojishughulisha na utoaji wa elimu kama vile shule za serikali na binafsi, Vyuo vikuu,Vyuo vya ufundi, vituo vya kutoa elimu.
AMKA TAFUTA MAARIFA!
Imeandaliwa na
Nobel Edson Sichaleh
Fasmo Tanzania
0783961492
Comments