Msingi Wa Lishe Bora katika shule mbalimbali
Mapema leo timu zetu ya Wataalamu wa lishe tulitembelea shule ya msingi Mwembesongo, Bungo na Mchikichini B zilizopo Morogoro mjini. Dhumuni kubwa la matembezi haya ni kutoa elimu na kukumbushana na wanafunzi pamoja na waalimu wao juu ya ulaji bora huku tukilenga zaidi kuhamasisha ulaji wa mboga za majani, samaki na maziwa ambavyo vinafaida lukuki mwilini.
Kwa mwanafunzi ni ngumu kula anavyotaka kwa kuwa kula kwake kuna tegemea wazazi, lakini akianzwa kujengwa kiakili juu ya ulaji wa afya pasi na shaka kadri anavyokua mkubwa ataishi ile elimu na kuwa na afya njema kwa kuwa atakuwa anakula vizuri kadri ya mahitaji ya mwili.
Wanafunzi wa shule zote zilizotembelewa na wataalamu wa Lishe wamekuwa wachangamfu na wasikivu wakati wa upataji wa elimu. Hii imechochea uelewa wao kuwa mzuri na kuzidi kuhamasika na ulaji wa afya.
Tutazidi kutembelea shule nyingine zaidi hapa mjini Morogoro ili kufanikisha wanafunzi wengi zaidi wanapata hii elimu kwa manufaa yao ya sasa na ya baadae, pia kwa manufaa ya taifa.
Taifa lenye magonjwa ni taifa dhaifu na masikini. Simama Nasi
#MLB2020
MSINGI WA LISHE BORA
#ShuleTanzania
https://www.instagram.com/p/CE9ip37gWvB/?igshid=c0t77jt6thcv
Comments