Wanajamii Wanahitaji Elimu

Jamii yetu bado inachangamoto nyingi sana. Na kwa bahati mbaya zipo changamoto ambazo zinahatarisha ubora wa kizazi kijacho kiafya na kimaadili.

Jambo zuri ni kwamba wanajamii wanazijua changamoto hizo japo sio kwa upana mkubwa. Kwa mfano wanajamii wengi wanajua lishe isipokuwa nzuri inaathiri afya lakini hawajui lishe mbovu ikoje na lishe bora ikoje. Wao miaka nenda miaka rudi watajilia kile kilichopo au kile wanachopenda. 


Haya twende kwenye malezi, huko nako changamoto chungu nzima. Wazazi na walezi wanajua malezi yasipokuwa mazuri yanaathiri moja kwa moja ukuaji, afya, tabia na hata masomo ya mtoto. Lakini malezi bora yamebaki kuwa changamoto kwe wengi.

Usimamizi mdogo wa wazazi, mawasiliano madogo/mabaya baina ya watoto na wazazi, vipigo vikubwa, matusi na matendo mbalimbali yanayowanyima watoto haki zao za msingi. 
Hatari iliyopo, matendo hayo mengi yamekuwa ndiyo mtindo wetu wa kawaida wa maisha hii inapelekea wazazi kutoambilika. Majirani nao kuchukulia kawaida au kuogopa kuripoti kwa kuwa kuna muda hata wenye mamlaka watalimaliza kikawaida (chinichini).




Hitaji kubwa kwao katika kutatua matatizo mengi ni Elimu na Mazingira wezeshi. Vitu ambavyo ni jukumu la kila mtu kusaidia uwezeshaji. Jamii yetu ina elimu nyingi potofu/potoshi na vikwazo vingi sana katika utafutaji wa utatuzi.
Kama viongozi wata wajibika na wananchi wataonyesha ushirikiano kama kujiyokeza kwenye mikutano na kutoa kero zao au maoni na yakafanyiwa kazi kwa uhakika na kwa muda shida nyingi zitapungua.
TUSIMAME KUJIKWAMUA.

Comments

Popular posts from this blog

Mitindo Yetu Ya Ulaji.

Nafasi ya Maziwa katika Afya Zetu.

MADHARA YA UTENGANO WA KIJAMII YALIYOSABABISHWA NA COVID19