Mradi wa MSINGI WA LISHE BORA katika Manispaa ya MOROGORO MJINI

MSINGI  WA LISHE BORA
Msingi wa lishe bora ni mradi wa utoaji elimu ya lishe kwenye shule za msingi katika manispaa ya Morogoro mjini. Mradi huu umelenga kuwajengea watoto tabia na maarifa ya kujua masuala ya msingi ya lishe yatakayowasaidia kufanya maamuzi sahihi katika ulaji bora na ulaji wa afya ili kuwaepuka kupata magonjwa na matatizo ya kiafya yanayohususiana na lishe kama kisukari, matatizo ya mifupa, matatizo ya moyo, matatizo ya ini na unene uliokithiri..

Maarifa hayo ni pamoja na kujua namna nzuri za kupangilia mlo kamili kwa kujumuisha makundi yote ya chakula, kuwajengea tabia ya usafi wa chakula na mwili, kuwafumbua akili juu ya vyakula vipi wasivipe kipaumbele kwenye milo yao kutokana na wingi wa vyakula hivyo hugeuka hatari kwenye afya zetu. 
Pamoja na hayo pia elimu juu ya vitu mbalimbali vya afya kama kuwafundisha ustaarabu wa mezani (table manners), mitindo mizuri ya kukaa ili kulinda afya ya mifupa na nyama pamoja na umuhimu wa Bima ya afya.
Morogoro mjini kuna shule za msingi 64 za serikali. Zimechaguliwa shule 25 kati ya 64 kuzifikishiwa hii elimu ya lishe kwa mwaka huu kama msingi wa kujiandaa kuzifikia shule zote (Binafsi na serikali) katika manispaa ya Morogoro mjini. Mradi huu utaenda sambamba na kuanzishwa kwa Lishe Clubs katika shule hizo.

Shule za msingi 25 zitafikiwa na mradi huu. Shule hizo ni
1. MTAWALA
2. MAFISA A
3. MAFISA B
4. MSAMVU A
5. MSAMVU B
6. MJI MKUU
7. MWEMBE SONGO
8. KALOLENI
9. KIKUNDI
10. MCHIKICHINI A
11. MCHIKICHINI B
12. BUNGO
13. KIWANJA CHA NDEGE
14. UHURU
15. SUA
16. MAFIGA A
17. MAFIGA B
18. MISUFINI A
19. MISUFINI B
20. MAZIMBU A
21. MAZIMBU B
22. MWERE A
23. MWERE B
24. MKWAJUNI
25. KILAKALA.
Mradi wa MSINGI WA LISHE BORA unalenga kuwafikia wanafunzi zaidi ya elfu saba (7000) ambao kati yao walengwa wakuu ni wanafunzi wa darasa la tano na darasa la sita. Elimu ya lishe itaanza kutolewa mwezi wa Septemba 2020 hadi Octoba 2020.

Ahsante!

Comments

Popular posts from this blog

Mitindo Yetu Ya Ulaji.

Nafasi ya Maziwa katika Afya Zetu.

MADHARA YA UTENGANO WA KIJAMII YALIYOSABABISHWA NA COVID19