Shairi: IWE LEO
IWE LEO Naomba iwe leo, Kesho mbona mbali? Tuwaongeze upeo, Wakulima kila mahali, Wapate maendeleo, Kwa sera za serikali. Furahisha wakaribu, Wambali watasogea, Serikali inayo sababu, Wakulima kutetea, Miaka wapata tabu, Hayupo kuwasemea. Bajetiye iwe nono, Wafikiwe vijijini, Wapanuliwe maono, Wasilime kizamani, Waachie la mkono, Wahifadhi ghalani. Jicho umwagiliaji, Sayansi shambani, Wapate mengi maji, Wasingoje mvuani, Waongeze uzalishaji, Tuwauzie majirani. Kilimo kipae thamani, Nao wakwae ukwasi, Walioko shambani, Waendelee kwa kasi, Wote wa masokoni, Uchumi wajinafasi. Miundombinu mazingira, Isiyotegemea misimu, Wapewe malengo dira, Vikundi wapate elimu, Kilimo kifanyike ajira, Kisiishie kuwakimu. Kweli kesho nayo siku, Lakini leo yawezekana, Tupitishe sera sumaku, Kilimo kiwavutie vijana, Wengi wakimbilie huku, Kilimo kiwe cha maana. Paza Sauti Wakulima Wanyanyuke Kiuchumi, Kiteknolojia na Kiuzalishaji. Imeandaliwa na, Nobel E Sichaleh. 0783961...