Posts

Showing posts from April, 2021

Je Mazingira ya Shule nchini yanachukua tahadhari kuwalinda watoto na magonjwa?

Image
Dunia ikiwa bado ikipambana na janga la Korona na nchi nyingi zikiwapatia wananchi wake chanjo na kulegeza sheria za tahadhari za kupambana na gonjwa hilo ambalo linaambukizwa kwa njia ya hewa. Baadhi ya nchi ziliwahi sana kuruhusu shughuli za masomo kwa wanafunzi wa shule za msingi hadi chuo huku zikitoa masharti ya kuzingatiwa wakati wa masomo.  Moja ya nchi hizo ni Tanzania, bila kutazama sana jinsi nchi yetu ilivyopambana na janga la Korona makala hii fupi imejikita katika kuangalia kwa makini mazingira ya shule hususani za msingi na sekondari jinsi yanavyoweza kulinda afya za wanafunzi au kuchochea maambuzi ya magonjwa mbalimbali yenye mfanano wa namna ya kuambukizwa na kukumba watu wengi.  Mazingira ya usafi wa madarasa, vyoo vya wanafunzi, uwepo wa maji tiririka ya kunawa na usafi kwa jumla kwa shule nyingi za msingi za serikali bado ni kitendawili. Hii kwa shule zote bila kujali eneo iliyopo, shule zilizopo mjini zina changamoto zake lukuki ikiwemo mazingira ya uuza