Misemo na Methali Zenye Uchakula
Kwenye maisha yetu ya kila siku tunaishi tuzizungumza. Tunazungumza kwa kutumia lugha yetu adhimu kabisa ya kiswahili huku tukiongelea vitu mbalimbali kwa lugha ya kawaida, lugha ya kimazingira na lugha ya kufikirika ili kufanikisha mawasiliano baina yetu. Katika maongezi yetu misemo na methali hutumika kwa sana katika kuwasiliana hii ni pamoja na kuonyana, kuhamasishana, kufarijiana na kuburudishana. Leo ikiwa ni siku nzuri kabisa nimeona vyema tufurahi pamoja kwa kukumbushana methali na misemo tunayoitumia kila siku kwenye jamii yetu lakini ina taswira yenye uchakula yani yenye imeelezea mazingira ya ulaji kama vile chakula, kinywaji, shamba au utafutaji. 1. Kuvunjika kwa mwiko sio mwisho wa kupika. 2. Chovya chovya humaliza buyu la asali. 3. Ukimchunguza sana bata hutomla. 4. Kipenda roho hula nyama mbichi. 5. Kikulacho kinguoni mwako. 6. Mwenye shibe hamkumbuki mwenye njaa. 7. Shibe mwana malevya, njaa mwana malegeza. 8. Kizuri kula na nduguzo. 9. Mbuyu ulianza kam...