Misemo na Methali Zenye Uchakula
Katika maongezi yetu misemo na methali hutumika kwa sana katika kuwasiliana hii ni pamoja na kuonyana, kuhamasishana, kufarijiana na kuburudishana.
Leo ikiwa ni siku nzuri kabisa nimeona vyema tufurahi pamoja kwa kukumbushana methali na misemo tunayoitumia kila siku kwenye jamii yetu lakini ina taswira yenye uchakula yani yenye imeelezea mazingira ya ulaji kama vile chakula, kinywaji, shamba au utafutaji.
1. Kuvunjika kwa mwiko sio mwisho wa kupika.
2. Chovya chovya humaliza buyu la asali.
3. Ukimchunguza sana bata hutomla.
4. Kipenda roho hula nyama mbichi.
5. Kikulacho kinguoni mwako.
6. Mwenye shibe hamkumbuki mwenye njaa.
7. Shibe mwana malevya, njaa mwana malegeza.
8. Kizuri kula na nduguzo.
9. Mbuyu ulianza kama mchicha.
10. Mgagana upwa hali wali mkavu.
11. Mchumia juani hulia kivulini.
12. Adui muombee njaa.
13. Mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu.
13. Mgema akisifiwa tembo hulitia maji.
14. Mkulima hachagui jembe.
15. Fuata nyuki ule asali.
16. Ukiona maziwa utadhani tui na ukiona tui utadhani maziwa.
17. Simba mwenda pole ndiye mla nyama.
18. Usidharau nazi embe tunda la msimu.
19. Kunguru hanenepi kwa jalala moja.
20. Mla vya wenzake na Chake huliwa.
21. Ukicheza na nyani utavuna mabua.
22. Ng'ombe hanenepi siku ya mnada.
23. Samaki mkunje angali mbichi.
24. Mwenye kisu kikali ndiyo mla nyama.
25. Ukila na Kipofu usimguse mkono.
Mpaka hapo nina imani methali na misemo mbalimbali imeshaanza kukujia kichwani mwako yenye mfanano wa chakula au mazingira ya ulaji.
1. Mgomba haulemewi na mkungu.
2. Kaokota dodo chini ya Mnazi
3. Usionee dagaa onea samaki.
4. Mzoea vya kunyonga hawezi kuchinja.
5. Mzoea kula nyama ukimpa samaki wamuonea.
6. Uloho ulimponza Fisi.
7. Simba akizidiwa hula nyasi.
8. Kitumbua kimeingia mchanga.
9. Ngumu kutafuna usimeze haraka
10. Njaa ni kipimo cha akili.
11. Kisichoridhiki hakiliki
12. Jungu kuu halikosi ukoko
Tukikutana ana kwa ana tutaitaja yote kwa pamoja na kwa wingi mkubwa. Lengo ni kuongesha tu namna ya mambo na majina ya vyakula yanavyotumika kufikisha ujumbe kwenye jamii au chakula kutumika kama tafsida au lugha ya picha katika kufanikisha uwasilishwaji wa ujumbe lengwa ili kujenga au kuburudisha jamii. Chakula ni kitamu kwa kula na ni kitamu kwenye lugha. Basi nimalizie kwa misemo hii michache
1. Mgonjwa wake uji
2. Shamba la bibi
4. Kunywa mtori nyama zipo chini
5. Wamemlisha matango pori
6. Maji mara moja kama maharage ya Mbeya.
7. Mchele mchele
8. "Anatema yai sana" ikimaanisha anaongea kingereza kizuri sana.
9. Mwindaji hapigi kelele.
Najua umeshaanza kupata misemo na methali zingine. Waweza weka kama maoni kwenye sehemu yetu ya maoni hapo chini na sisi tutaziongeza kwenye makala hii.
Imeandaliwa na
Nobel Edson
Mwanalishe
0783961492
Comments