Posts

Showing posts from November, 2021

Yakimbie Magonjwa Sugu Yasiyoambukizwa.

Image
Tupo ndani ya mwezi wa kuadhimisha kujikinga na kupambana na magonjwa sugu yasiyoambukiza. Maadhimisho haya haswa huanza tarehe 6 hadi 13 mwezi Novemba kila mwaka ambapo hiyo wiki huwa ni kilele chake.  Lengo la maadhimisho haya ni kuifahamisha na kukumbusha jamii uwepo wa magonjwa haya hatari na kujua jinsi ya kujikinga na kuyatibu. Magonjwa yasiyoambukiza ni magonjwa yote ambayo hayawezi kuambukizwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine. Mara nyingi huwa ni ya kudumu na ni matokeo ya muunganiko wa sababu za kijenetiki, mazingira, tabia pamoja na fiziolojia (ufanyaji kazi wa sehemu mbalimbali za mwili wa mtu).  Mfano wa magonjwa haya ni kama magonjwa ya mfumo wa mzunguko wa damu (kiharusi na mshtuko wa moyo), kisukari, saratani na magonjwa katika mfumo wa upumuaji kama vile athma (asthma). Magonjwa mengine ni kama magonjwa ya akili, majeraha, selimundu na ulemavu.  Kati ya magonjwa haya, magonjwa katika mfumo wa mzunguko wa damu yanaongoza kusababisha vifo vya watu wengi zaidi dun