Mfumo wetu wa mmeng’enyo wa chakula, je umesahaulika?
Mfumo wetu wa mmeng’enyo wa chakula, je umesahaulika? Ukikaa ukaangalia mambo mengi kwa makini utaona kwamba watu wengi huangaika na uzuri wa sehemu za miili yao wanazoziona. Ndio maana utakuta kuna huduma nyingi sana zinazohusu kutengeneza kucha, nywele (almaarufu kama saluni), kufanya maseji ya sehemu mbalimbali za mwili, skrabu. Ingawa huduma za afya zipo maeneo mengi lakini huduma ya uchunguzi ya mfumo wa chakula haipewi kipaumbele kama sehemu kubwa ya inayoweza kutumika kutatua matatizo mengi ya afya yanayoisibu jamii. Ni mara chache sana watu wengi wakipatwa na shida za kiafya hufikilia kuhusu afya ya mfumo wa mmeng’enyo wa chakula. Hii sio kibongo bongo tu bali hata nchi za wenzetu suala hili halipewi kipaumbele na watu wa kawaida pamoja na wale walioelimika katika sekta ya afya (wataalamu wa lishe, madaktari, wafamasia n.k) Hii ina maana kwamba kuna uwezekano mkubwa, matatizo mengi ya afya zetu yanaweza yakawa yanatokana na shida zilizopo katika mfumo huu kwa unafanya kazi kubw...