Mitindo Yetu Ya Ulaji.
MITINDO YA ULAJI Viumbe hai vyote akiwemo na mwanadamu huitaji chakula ili kuishi. Mwanadamu ana mahitaji makuu matatu na chakula ni hitaji muhimu zaidi ya mengine ambayo ni mavazi na malazi. Kwa umuhimu wa chakula, mwanadamu huitaji kula kila siku. Na inapotokea hajala au kavusha mlo kuna utofauti hujisikia. Utofauti huo waweza kuwa upungufu wa nguvu mwilini, kizunguzungu, na wengine hujisikia uwepesi wa mwili. Wewe ukishikwa na njaa unakuwaje au tabia gani hujitokeza? Watu wanamitindo mbalimbali ya ulaji. Mitindo ya idadi ya milo, wakati wa kula, aina ya vyakula na kiasi cha chakula na hii hutokana na sababu kadhaa. Sababu kama za kiuchumi, mazoea, ratiba ya mtu, sababu za kidini, umri, hali ya mwili na kiafya ya mtu husika pamoja na mazingira na upatikanaji wa vyakula. Kama picha inavyoonyesha hapo watu 4500 walioonyesha wao hula milo mingapi ndani ya masaa 24 yani milo kwa siku. Wapo wa mlo mmoja hadi milo minne na kuendelea. Kwani wewe unakula milo mingapi kwa siku na kwa nini? Wa...