Posts

Showing posts from 2023

Mtoto wa Afrika

Image
Siku ya Mtoto wa Afrika. Ni leo tarehe 16 mwezi Mei siku ambayo Tanzania na nchi zingine za Afrika zinaungana kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika.  Kauli mbiu ya mwaka huu ni  "Maendeleo Endelevu 2030: Imarisha Ulinzi na Fursa Sawa kwa Watoto” Kauli mbiu hii inawahimiza wazazi, walezi, jamii, Serikali na wadau wengine kuzingatia wajibu wetu katika kuimarisha mifumo ya ulinzi na maendeleo ya Mtoto ili aweze kudhibiti changamoto ya ongezeko la vitendo vya ukatili nchini pamoja na kutoa haki sawa kwa watoto wote bila ubaguzi wa aina yoyote. Awali ya yote, chimbuko la Maadhimisho haya ni Azimio lililopitishwa na uliokuwa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU) mwaka 1990 kwa lengo la kuwakumbuka watoto wa kitongoji cha Soweto nchini Afrika ya Kusini waliouawa tarehe 16 Juni, 1976 kutokana na ubaguzi wa rangi. Watoto hao walikuwa wakidai haki zao za kutobaguliwa pamoja na haki nyingine za kibinadamu ikiwemo haki ya kupata elimu bora na hivyo kupinga mifumo ya elimu ya kibaguzi. Kufuatia tuk...

Siku ya Maziwa Duniani. Tusherekee au Tusimame na Kujitafakari?

Image
MAZIWA MAZIWA MAZIWA! Tulipokuwa shuleni tulijifunza makundi ya Wanyama kulingana na sifa zao. Moja ya kundi hili ni mamalia ambao sifa yao kuu ni Wanyama wanaonyonyesha akiwemo popo, binadamu, mbwa, ng’ombe, mbuzi, kondoo nk. Wanyama hawa hufanya hivi kwa kipindi Fulani na kuacha kunyonyesha mtoto/watoto wao. Kwa mfano, ndama wa ng’ombe haachishwa akiwa na umri wa miezi 4 hadi 5, baadhi ya jamii za nyani huendelea kunyonyesha watoto wao hadi wanapofikia umri wa miaka 4 wakati tembo huendelea kumnyonyesha mtoto wake hata akiwa na umri wa Zaidi ya miaka 2. Hii ina maanisha kila mnyama anaezalisha maziwa ni kwa ajili ya mtoto/watoto wake tu. Pia tutakubali kuwa kila mnyama ana tabia zake katika kumuachisha mtoto wake kunyonya. Kwa binadamu, inashauriwa mtoto anyonyeshwe hadi atakapotimiza umri wa miaka 2 na ikiwezekana aendelee kunyonyeshwa, ingawa watu wengi hawafanyi hivyo. Wengine huishia mwaka mmoja na nusu na kuacha kumnyonyesha mtoto wake. Leo ni kilele cha maadh...

Mfumo wetu wa mmeng’enyo wa chakula, je umesahaulika?

Image
Mfumo wetu wa mmeng’enyo wa chakula, je umesahaulika? Ukikaa ukaangalia mambo mengi kwa makini utaona kwamba watu wengi huangaika na uzuri wa sehemu za miili yao wanazoziona. Ndio maana utakuta kuna huduma nyingi sana zinazohusu kutengeneza kucha, nywele (almaarufu kama saluni), kufanya maseji ya sehemu mbalimbali za mwili, skrabu. Ingawa huduma za afya zipo maeneo mengi lakini huduma ya uchunguzi ya mfumo wa chakula haipewi kipaumbele kama sehemu kubwa ya inayoweza kutumika kutatua matatizo mengi ya afya yanayoisibu jamii. Ni mara chache sana watu wengi wakipatwa na shida za kiafya hufikilia kuhusu afya ya mfumo wa mmeng’enyo wa chakula. Hii sio kibongo bongo tu bali hata nchi za wenzetu suala hili halipewi kipaumbele na watu wa kawaida pamoja na wale walioelimika katika sekta ya afya (wataalamu wa lishe, madaktari, wafamasia n.k) Hii ina maana kwamba kuna uwezekano mkubwa, matatizo mengi ya afya zetu yanaweza yakawa yanatokana na shida zilizopo katika mfumo huu kwa unafanya kazi kubw...