Posts

Showing posts from April, 2024

Afya ya Akili na uharifu katika Jamii.

Image
Siku moja tutaandaa jukwaa litakayoelezea namna afya ya akili inavyochochea uharifu katika jamii. Matukio mengi ya kiharifu yatokeayo kwenye jamii na yanayoripotiwa polisi yanachangiwa sana na matatizo ya kiakili ya wanajamii kuliko umaskini, tamaduni, sera na umiliki wa silaha. Na, Charles Msigwa.

Shairi: IWAJE?

Image
Wewe ulitakaje? Shule za msingi Vitu vifanyikaje? Katikati ya vipindi Watoto walaje? Kwa elimu-ushindi Mimi kama wewe Nina uwezo kufikiri Nafikiri mwenyewe Siwezi shikiwa akili Mwenye haki apewe Vinginevyo ni ukatili Haki ya kuelimika Na malezi stahiki Hakizo kuzishika Mtoto huwa rafiki Mzaziye wajibika Utajaona mantiki Mapumziko wasile! Darasani waingie Njaa iwazingile Somo lisiwaingie Shule waikimbie Maoniyo niambie? Wale chakula vizuri Darasa changamfu Wasipate tena sifuri Utoro ugeuke hafifu Wawe watoto wazuri Wenye afya nadhifu. Changia mawazo Tupate mwongozo Tuwajengee uwezo Elimu bora ni nguzo Hatua hizi mwanzo Tuvishinde vikwazo