TUNAWEZA ISHI BILA TUMBAKU.
Tarehe 31 Mei ya kila mwaka ni siku ya kupinga matumizi ya sigara na bidhaa za Tumbaku Duniani (World No Tobacco Day). Siku hii iliasisiwa na Shirika La Afya Duniani (WHO) mwaka 1987. Hii ni kutokana na madhara ya bidhaa hizo kwa watumiaji na watu wanaowazunguka kiafya na kimazingira. Madhumuni ya siku hii ni kuhamasisha watu na kutoa elimu juu ya madhara yatokanayo na uvutaji na utafunaji wa tumbaku. Utengenezaji na uvutaji wa sigara ni halali hapa nchini kwetu Tanzania. Utafiti unaonyesha kwa siku duniani watu takribani 500 hufariki dunia kutokana na matumizi ya tumbaku. Tumbaku inaweza kuzalisha aina mbalimbali za saratani, magonjwa ya moyo, kiharusi, vidonda vya tumbo na magonjwa sugu ya kifua. Utafiti uliofanywa hapa nchini unaonyesha asilimia 40 hadi 50 ya watu wanaougua ugonjwa wa saratani ya mapafu unatokana na uvutaji wa tumbaku. Katika hilo hata wasiotumia tumbaku wamekuwa wakiathirika zaidi kutokana na kuvutishwa bila ridhaa yao, kutokana na ukwe...