Huduma ya Kangaroo Katika Malezi ya Mtoto
Huduma ya Kangaroo katika malezi ya mtoto
Mgusano wa ngozi kwa ngozi kati ya mzazi na mtoto maarufu kwa jina la "Huduma ya Kangaroo" ni huduma ambayo wazazi hususani akina mama huwapa watoto wao kipindi wakiwa wachanga. Huduma hii inafaida kubwa kwa watoto na kwa wazazi pia, kwa kuwa inaongeza ukaribu kati yao.
Maneno "huduma ya kangaroo" ilikuwa inaitwa kwa kufanana kwake na jinsi Kangaroo hubeba watoto wao. Huduma ya ngozi kwa ngozi huiga mazingira ya kinga na ya uleaji ya mfuko wa kangaroo. Kwa ufafanuzi, utunzaji wa kangaroo ni utunzaji wa maendeleo kwa kugusanisha ngozi ya watoto wachanga dhidi ya kifua cha mama au baba.
Huduma ya kangaroo ilianza katika miaka ya 1970, kama njia ya kukuza utunzaji na kunyonyesha mapema kwa watoto wachanga wa waliozaliwa ndani wa muda. Mwishoni mwa 1970, shughuli hii ilipanuliwa kwa watoto wachanga waliozaliwa kabla ya miezi tisa kutokana na viwango vya vifo vingi, viwango vya juu vya maambukizi na ukosefu wa rasilimali, kama vifaa vya joto. Huduma ya kangaroo hutumiwa mara nyingi katika kitengo cha watoto wachanga (NICU) ulimwenguni kote, kwa sababu ya faida zake kubwa kwa mama na mtoto. "
Wazo la ngozi-kwa-ngozi ni kama utunzaji wa kangaroo, na katika hali nyingi, maneno hutumiwa kwa kubadilishana. katika siku za sasa, ngozi-kwa-ngozi kawaida ni neno linalotumiwa kwa watoto wachanga waliozaliwa ndani ya muda, kuelezea ni saa ngapi na siku za kwanza za maisha ya mtoto mchanga zinatumika dhidi ya kifua cha mama, kukuza utengenezaji wa maziwa na maziwa. Huduma ya kangaroo hutumiwa mara nyingi wakati wa mtoto kazaliwa kabla ya miezi tisa katika kitengo cha cha watoto wachanga NICU.
Hapa nchini kwetu Tanzania hospitali nyingi kubwa zina vitengo vinavyoruhusu wamama hususani wale waliojifungua watoto kabla ya miezi tisa. Kwa mfano Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Mbeya ina kitengo kinaitwa "Kangaroo Care Unit" ambapo watoto wanaozaliwa kabla ya muda wanakuwa kwenye chumba chenye vifaa vya kumpatia joto, mama zao wanaenda kuwanyonyesha na kuwapa huduma ya kangaroo na kisha kiwarudisha kwenye vyumba hivyo mpaka utakofika muda wa kuwaruhusu kwenda nao nyumbani. Pia watoto waliozaliwa baada ya miezi tisa wazazi wao hushauriwa kuwapatia hiyo huduma kwa manufaa mapana kati yao.
Faida ya Huduma ya Kangaroo
Huduma ya Kangaroo hutoa faida za kifiziolojia na kisaikolojia, kwa watoto wachanga na wazazi. Huduma ya kangaroo inaweza kufanyika wakati wowote wa siku, mara kwa mara kama vile mtoto huvumilia. Inapendekezwa kila siku, kwa muda wa lisaa, lakini kiasi chochote cha muda kinaweza kuwa na faida.
Faida za Huduma ya Kangaroo kwa watoto wachanga
●Ustamilivu wa Kifiziolojia (udhibiti wa joto na mkandamizo wa damu, ustamilivu wa mapigo ya moyo na upumuaji)
● Ukuaji wa Ubongo, utambuzi na maendeleo ya mwili.
● Uboreshwaji wa utendaji kazi wa mfumo wa kinga ya mwili
●Kuongezeka kwa uzito
●Ulalaji mzito na mzuri na wa muda mrefu.
●Kuongezeka kwa ukaribu na mzazi na kupungua kwa mafadhaiko na kulialia
Faida za Huduma ya Kangaroo kwa Mzazi
●Ukaribu, mawasiliano na muunganiko na mtoto
●Huboresha hisia na mwitiko kwa mtoto
● Huongeza ujasiri katika kumuhudumia mtoto na Kumtoa mtoto hospitali kumpeleka nyumbani
●Huongeza uzalishaji wa maziwa ya mama
●Huleta mafanikio au wepesi wakati wa kumnyonyesha mtoto. Mtoto anakuwa hasumbui.
Watoto wachanga huvutiwa sana na sauti ya mapigo ya moyo wa mama zao au baba zao. Ikiwa mtoto wako ni mtata, jaribu kumfunika na blanketi lenye joto huku umemlaza kifuani mwako na upunguze vishawishi vya nje. Kwa watoto wachanga waliozaliwa kabla ya wakati, kutikisa na kupigwapigwa kunaweza kuchochea zaidi na lakini pia kunaweza kumfanya mtoto kuchoka, na kupunguza faida ya huduma ya kangaroo.
Kwa msaada wa makala za Gebauer-Steinick, Mtaalamu wa malezi ya watoto
Na
Nobel Edson Sichaleh
Fasmo Tanzania
0783961492
Comments