MADHARA YA UTENGANO WA KIJAMII YALIYOSABABISHWA NA COVID19

Madhara ya Utengano wa Kijamii yaliyoletwa na COVID19

Nchi nyingi sasa duniani zimeanza kulegeza masharti ya tahadhari zilizowekwa zifuatwe ili kupunguza na hata kutokomeza maambukizi na madhara ya janga la virusi vya Korona. Ugonjwa wa Korona umeleta madhara mengi ya muda mfupi na mengine ya muda mrefu. Itachukuwa muda jamii yetu kurudi kwenye maisha ya kawaida, kiuchumi na kimahusiano baina ya watu hili ni kutokana na tahadhari tunazochukua na tulizochukua katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Covid19.
Leo naomba tuzungumzie madhara ya muda mfupi na muda mrefu ya Kujitenga kijamii (Social distancing/Isolation ).
Kujitenga kijamii ni moja ya njia iliyobuniwa na kuhamasishwa itumike katika kuzuia maambukizi ya Corona. Njia hii ililenga mtu kukaa umbali wa Mita moja na zaidi na hata kujifungia ikiaminika umbali huo mtu aongeapo au akikohoa virusi haviwezi kumfikia mwingine kwenye huo umbali.
Njia hii imekuwa na msaada kwa kupunguza kasi ya maambukizi ndani ya wanajamii kwenye familia na mikusanyiko kama sehemu za ibada. 

Licha ya faida kubwa ya njia hii lakini pia imekuwa na madhara makubwa kwa jamii yetu iliyojengeka katika misingi ya undugu na upendo. Kutosalimiana kwa kushikana mikono, kutokukumbatiana, kutotumia muda mwingi katika mazungumzo kama ilivyozamani. Wanasaikolojia wanasema hali hii imeleta upweke, msongo wa mawazo.

Upweke
Wazee huwa katika hatari kubwa wakati wa kutengwa. Utafiti umeunganisha kutengwa kwa jamii na upweke katika wazee na hatari kubwa ya hali anuwai ya kiakili na kifikra, na pia kupungua kwa utambuzi na magonjwa yanayoenda kuathiri nevu hata kupelekea kifo cha mapema. Pia upweke kwa wanajamii wengine waliozoea kukutana na kufurahi pamoja katika maeneo yao ya kazi, shule, na vijiweni.

Kuweweseka Usiku
Kumekuwa na ripoti za watu ambao wana ndoto za ajabu usiku au shida ya kulala kwa sababu ya janga linalozunguka la virusi vya Korona.
Achilia mbali mawazo lakini pia watu waliozoea kulala pamoja leo akilala bila mwenzake karibu kwa hofu ya maambukizi kuna athiri usingizi wake na hata ndoto zake. Hii sio mshangao. kulingana na utafiti juu ya jambo hili, kitu chochote ambacho kinaweza kusababisha wasiwasi au kufadhaika kitakuongeza hatari yako ya kuwa na ndoto za  ajabu usiku. Matukio ya kiwewe na ya kutisha pia yanaweza kuwa na athari kama hiyo kwa usingizi wako na ndoto zako.
Msongo wa mawazo na masononeko
Taarifa za kutisha juu ya kasi ya maambukizi na vifo vinavyotokana na Corona kumepelekea msongo wa mawazo kwa watu wengi vijana kwa wazee. Inapotokea mpendwa wao kafariki mazishi ya mpendwa yanakuwa yenye maumivu sana, wafiwa hamruhusiwi kukumbatiana na idadi ndogo sana ya watu katika maombolezo na mazishi au hata hamshiriki kwenye mazishi ya mpendwa wenu. Hili jambo linaleta mrundikano wa mawazo ukimjulisha na mawazo ya lini hili janga litaisha?? Vipi lisipoisha hivi karibuni? Vipi shughuli zangu za kimaisha? Nk
Uchangamfu hafifu
Kutokana na utengano wa kijamii watoto wengi hujikuta wamefungiwa ndani bila kucheza na wenzao kwa hofu ya maambukizi. Kitendo cha mtoto mdogo kutokuwa katika mazingira ya kucheza na kujichanganya na wenzake kunamfanya akili yake idumae na asiwe mchangamfu na mbaya zaidi kama hali ya kuwekwa mbali na wenzake itadumu kwa muda mrefu mtoto hujenge tabia ya kujitenga huko ukubwani. Uchangamfu hafifu wa mwili na akili kwa mtoto kunasabisha awe mzito katika kufikiria na kujifunza vitu hususani lugha.

Uwepo wa Hofu
Ikiwa Korona bado haijatoweka duniani basi ni wazi binadamu tunaendelea kuogopana kusogeleana kwa muda zaidi. Hofu hii inajengeka kwa kuhisi mtu yeyote anaweza akawa nayo na kuniambukiza. Ile tabia yetu ya kusalimiana kwa kushikana mikono hata kama hatufahamiani haitarudi kwa haraka tutaogopana kwa muda zaidi. Hofu inaufinya uhuru wetu wa kuishi kwa kujiachia na mazoea tuliyojijengea.

Kupungua kwa Ujamii
Jamii inaundwa na watu wanaokaribu na kushirikiana katika vitu mbalimbali. Utengano wa kijamii unapunguza ule ujamii wetu. Jamii inahitaji ukaribu ili tuitambue kama jamii, utengano au umbali wowote kati ya wanajamii kunapunguza ujamii wao. Jamii inatamaduni zake kama tamaduni vitaingiliwa na utengano wa kijamii ni wazi ujamii utapungua. Jamii ya michezo haijatimia bila mashariki wa mchezo huo, mchezo bila uwepo wa mashabiki unakosa radha. 
Jamii ya Watanzania wao ukisema wakae mita moja mbali na mwingine basi misiba yao itakuwa na maumivu zaidi kwakuwa wamezoea kuwa karibu kufarijiana.

Mambo yakufanyika ili kupunguza athari na madhara ya utengano wa kijamii
●Kukubali maisha lazima yaendelee
●Matangazo ya kuzidi kutoana hofu yazidi kuwafikia watu wengi zaidi ili hofu iondoke na maisha yarudi kama kawaida. Hilo ni pamoja na kutangaza hali ya ugonjwa nchini.
●Kila mmoja awe rafiki kipenzi wa mwingine. Tupigiane simu, tutembeleane kwa sana kuliko hata awali ili kuondoa upweke na hisia za kutengana
● Kuepuka maeneo yanayoleta hofu inaweza ikawa masokoni au daladala ili awe mtu awe huru na mwenye furaha kwenye mazingira anayohisi yana usalama kwa afya yake.

Yote kwa yote tuzidi kuchukua hatua sahihi kujikinga na Corona. USIOGOPE.... USIPUUZIE!!

Na 
Nobel Edson Sichaleh
Fasmo Tanzania
0783961492

Comments

Charles Msigwa said…
Makala Nzuri sana��
Unknown said…
Ni nzuri sana cha muhimu ni kuondokana na hofu pia tuwe wamoja sana kwapamoja twaweza kujikinga
Fasmo Tanzania said…
Ahsante kwa msisitizo uliotoa

Popular posts from this blog

Mitindo Yetu Ya Ulaji.

Nafasi ya Maziwa katika Afya Zetu.