USALAMA WA CHAKULA NI SUALA LA KILA MTU

Mpendwa msomaji wa makala zetu, tunayofuraha kukukaribisha tena kwenye blog yetu siku ya leo tarehe 7 Juni ambayo pia ni siku ya kuhadhimisha Usalama wa Chakula Duniani.
Chakula ni kitu chochote kinachoweza kuliwa na kuupatia mwili virutubishi na kinakubalika kijamii. Tunaposema kukubalika kijamii ni kama vile panya anakubalika kama chakula kule Mtwara lakini sio Chakula Mbeya kwakuwa jamii ya watu wa Mbeya haikubali ulaji wa panya.  Kuna vyakula aina mbalimbali lakini vyote vimegawanywa katika makundi matano kutokana na mfumo na kazi ya chakula mwilini.

Usalama wa chakula ni kutokuwepo kwa hatari au viwango vinavyokubalika vya hatari katika chakula ambayo inaweza kuumiza afya ya watumiaji. Hatari inayosababishwa na chakula inaweza kuwa ya kimelea, ya kemikali au ya asili na kawaida haonekani kwa jicho wazi: bakteria, virusi, au mabaki ya wadudu ni baadhi ya mifano .
Usalama wa chakula ni jukumu muhimu katika kuhakikisha kuwa chakula kinakaa salama katika kila hatua ya mlolongo wa chakula - kutoka uzalishaji hadi mavuno, usindikaji, uhifadhi, usambazaji, njia yote ya kuandaa na matumizi.
Magonjwa mengi yanayosababishwa na chakula kila mwaka, chakula kisicho salama ni tishio kwa afya ya binadamu na uchumi, kwa kawaida huathiri watu walio hatarini na waliotengwa, haswa wanawake na watoto. Idadi ya watu walioathirika na migogoro, na wahamiaji. 
Wastani wa watu milioni tatu ulimwenguni kote katika nchi zilizoendelea na zinazoendelea hufa kila mwaka kutokana na ugonjwa wa chakula na maji. Chakula ndio kianzio cha nguvu zetu, afya zetu na ustawi wetu. Sisi mara nyingi huchukua hatua kuwa ni salama, lakini katika ulimwengu unaoendelea kuwa mgumu na unaounganika ambapo minyororo ya thamani ya chakula inakua kwa muda mrefu, viwango na kanuni ni muhimu zaidi kwa kutunza salama.

Usalama wa chakula ni suala la kila mtu.
Kuanzia kwa mkulima mpaka mlaji wote tunawajibika katika kuhakikisha usalama wa chakula. Uzalishaji wa chakula shambani na viwandani hadi katika ngazi ya upishi na uandaaji tayari kwa kuliwa usalama ni jambo muhimu.
Serikali, viwanda, wasambazaji wa chakula, wafanyabiashara masokoni na kwenye maghala wote kwa pamoja wanajukumu la kuhakikisha usalama wa chukula. Usalama wa chakula ni kuanzia kuhakikisha uwepo wa chakula cha kutosha. Uwepo wa chakula cha kutosha ni kuhakikisha uzalishaji wa chakula ni mkubwa pia utunzaji wa chakula ni mzuri ili kuhakikisha chakula hakipotei au kuharibika. 
Kutokana na kila mmoja wetu kuhitaji chakula kwenye mwili hivyo usalama wa chakula sio wa watu fulani bali ni wa wote. Wote tunawajibu wa kuhakikisha usafi wa chakula kabla hatujala kama vile kuosha, kupepeta, kumenya na kuchuja. Pia kusoma lebo kujua tarehe ya kutengenezwa na kuisha muda wake. Yeyote atakayepuuzia nafasi yake katika kuhakikisha usalama wa chakula anaweza kupata madhara au kusababisha madhara ya kiafya na kiuchumi kwa watu wengine.

HALI YA CHAKULA DUNIANI
Baada ya miongo kadhaa ya kushuka kwa kasi, njaa ya ulimwengu imekuwa ikiongezeka tangu mwaka 2015. Takriban watu milioni 821 duniani waliteseka na njaa mnamo 2018. Ikiwa hakuna kitakachobadilika, changamoto kubwa ya kufanikisha Lengo la "HAKUNA NJAA" ifikapo mwaka 2030 hautapatikana. Wakati huo huo, kuzidi kwa ugonjwa wa kunenepa kupita kiasi unaendelea kuongezeka katika sehemu zote za dunia, kulingana na ripoti za Hali ya Usalama wa Chakula na Lishe Duniani 2019 .
Chakula na ugonjwa wa Korona
Kwa sasa, hakuna ushahidi kwamba virusi vya Korona ambavyo husababisha COVID-19 vinaweza kupitishwa kupitia chakula. Virusi huambukizwa hasa na watu, ambao wameambukizwa kupitia kukohoa na matone ya kupiga chafya, ambayo huchukuliwa na mtu mwingine. njia bora ya kuzuia COVID-19 ni kupitia njia bora za usafi, pamoja na uzalishaji  na uaandaaji mzuri wa chakula na matumizi yake.

Chakula kiwe salama,
Usafi tuzingatie,
Tumbo halitalalama,
Lishe bora tujipatie,
Tukiwekee alama,
Kisichofaa tusitumie.

Mkulima ukitoka kuvuna,
Mavuno hifadhi vizuri,
Pindi yatapokuwa hakuna,
Ghala lako lisiwe sifuri,
Utaendelea kutafuna,
Na kuendelea na zingine shughuli.

Makala hii ni kwa msaada mkubwa wa ripoti za Umoja wa Mataifa.

Na
Nobel Edson Sichaleh
Fasmo Tanzania 

Comments

Anonymous said…
Imekaa poa sana

Popular posts from this blog

Mitindo Yetu Ya Ulaji.

Nafasi ya Maziwa katika Afya Zetu.

MADHARA YA UTENGANO WA KIJAMII YALIYOSABABISHWA NA COVID19