Posts

Showing posts from July, 2020

UZITO ULIOKITHIRI

Image
UNENE AU UZITO ULIOKITHIRI NI HATARI  Kuwa na unene au uzito uliokithiri ni chanzo cha matatizo mengi ya kiafya hasa magonjwa yasiyo yakuambukizwa kama vile; kisukari, saratani na shinikizo kubwa la damu.  Takwimu zinaonyesha zaidi ya watu bilioni mbili duniani wameathiriwa na fetma (obesity) na zaidi ya vifo milioni nne vinasababishwa na fetma.   Katika nchi ya Tanzania takwimu za vifo vinavyotokana na magonjwa yasiyo yakuambukizwa (NCD) kutoka katika Shirika la Afya duniani (WHO) zinaonyesha vifo 134,600 kwa mwaka hutokana na magonjwa yasiyo yakuambukizwa (NCD), ambayo ni sawa na asilimia thelathini na tatu (33%) ya vifo vyote, hutokana na magonjwa yasiyoyakuambukizwa, na vifo hivi vimekuwa vikiongezeka kila mwaka   Kitaalamu njia ambayo ni salama zaidi mtu anapotaka kupunguza uzito au unene ni ile inayohusisha ulaji sahihi wa vyakula unaozingatia kanuni, ufanyaji wa mazoezi na kanuni mbalimbali za afya ambazo zimekuwa zikielezewa ...

DHANA ZA MAHUSIANO KATI YA MZAZI NA MTOTO KATIKA MALEZI.

Image
Tangu zamani kumekuwa na dhana na fikra mbalimbali katika jamii juu ya ukaribu wa mzazi na mtoto katika malezi na makuzi. Fikra na dhana hizi bado zipo kwenye jamii zetu kati ya familia na familia. Wapo wanaoamini mzazi hapaswi kuwa na urafiki na mtoto. Mzazi akiwa na urafiki na mtoto kuna mfanya mtoto awe kiburi na dharau kwa watu wengine kwa kuwa anajua mzazi ni rafiki yake atamtetea. Na muda mwingine urafiki huo hujenga mazoea kisha mtoto huwa na dharau kwa mzazi husika "Mazoea huleta dharau".  Dhana hii ni kubwa na maarufu sana kwenye familia nyingi za Kiafrika. Baba awe Baba na sio rafiki wa mtoto, baba inabidi aogopwe na kuheshimiwa sana na mtoto na sio mtoto akimuona baba aanze kumchezeachezea. Ni hii dhana ambayo wazazi wetu wengi wamekulia na imejenga nidhamu kubwa kati yao kwa kuwa kuna mstari mwekundu ulikolezwa (Red bold line) kati ya mtoto na mzazi.  Pia kundi lingine linabeba dhana ya MZAZI LAZIMA UWE RAFIKI MKUBWA WA MWANAO. Kundi hili l...

Mpango Binafsi wa Afya.

Image
Tanzania ni moja ya nchi zilizopo kusini mwa jangwa la sahara zenye idadi kubwa ya watu. Licha ya serikali ya Tanzania kufanya jitihada nyingi katika kupambana na maadui watatu ambao ni Ujinga, umasikini na Maradhi bado kuna changamoto kubwa kwenye jamii za Kitanzania hususani kwenye afya na lishe. Watu wengi bado hawana elimu toshelezi juu ya ulaji bora na mitindo mizuri ya maisha itakayowaepusha na matatizo ya kiafya na kilishe. Idadi kubwa ya Watanzania bado ina jikongoja katika kukamilisha milo mitatu kwa siku. Huku idadi kubwa zaidi ikiwa bado gizani katika kupangilia makundi ya vyakula katika mlo. Yote haya yanasababishwa na ukosefu wa elimu ya lishe kwa sehemu kubwa na pia umasikini unachangia kwa sehemu hali kuwa mbaya zaidi. Kwa kuwa wapo wenye uwezo wa kula watakavyo (idadi kubwa ya milo) lakini bado hawaipangilii vizuri. Changamoto nyingine iliyopo kwenye afya na lishe kwa Watanzania wengi ni ukosefu wa tamaduni au tabia ya kuzingatia kanuni za mambo mbalimbali. Maisha yetu ...

Shairi: TUISHINDE CHUKI

Image
Tuishinde Chuki Nasaha lukuki, Leo tusemezane, Tuishinde chuki, Mbinu tupeane, Isilete taharuki, Mwisho tuuane. Chuki roho chafu, Hasara abadani, Watu waliodhaifu, Huitunza kifuani, Tabia ya siafu,  Kujitia hatiani. Chuki mitaani, Imefika bungeni, Imeingia kanisani, Upendo pembeni, Tupendane jamani, Itasaidia mbeleni. Alimchukia Sadiki, Akapanga mpoteza, Kumvamia alidiriki, Ghafla akateleza, Akapoteza umiliki, Sasa magereza. Chuki huleta aibu, Hilo jambo jua, Waumbuka kiajabu, Waangukia pua, Utaishi kwa taabu, Utawaza jiua. Ndugu twachukiana, Sisi kwa sisi, Kutwa twawindana, Twaishi kifisi, Twashindwa samehana, Tumejawa ubinafsi. Samehe mara sabini, Na ukiweza sahau, Zinashauri dini, Kumbuka hilo mdau, Tukirudi vumbini, Upendo utawale walau. Tusamehane ndugu, Chuki ndani ondoa, Yaweza geuka rungu, Kisha uhai ikakutoa, Haimpendezi Mungu, Hakika yatutia doa. Na Nobel Edson Sichaleh Fasmo Tanzania

FAIDA ZA KUFANYA UCHUNGUZI WA KIAFYA MARA KWA MARA

Image
Faida za kufanya uchunguzi wa kiafya mara kwa mara . Kuna kampeni nyingi zinazohamasisha watu kufanya uchunguzi wa afya zao juu ya gonjwa fulani au hata juu ya hali ya afya ya mwili wote kwa ujumla. Kampeni kubwa ni za kuhamasisha kupima Virusi Vya Ukimwi (VVU) pia kupima chanzo cha homa "Sio kila homa ni Malaria". Pamoja na hayo kuna kampeni nyingi za kuhamasisha wanawake kupima hali zao afya hususani kwenye mifumo ya uzazi (saratani ya matiti na shingo ya uzazi) Licha ya jitihada nyingi za kuhamasisha watu kupima na kujua hali zao za kiafya zinazofanywa na serikali pamoja na asasi za kiraia lakini bado muamko wa watu umekuwa mdogo.  Sababu zinazofanya muamko uwe mdogo ni pamoja na hali ya uchumi, wengi kipato chao ni kidogo kiasi hata kupata milo mitatu ni mtihani.  Sababu zingine ni pamoja na uelewa mdogo juu ya umuhimu wa kuchunguza afya zao, baadhi ya Bima za Afya haziruhusu uchunguzi wa kiafya kwa asiye mgonjwa.  Utaratibu ni kwamba huwezi kupima magonjwa mbalimbali kam...

OUR SOCIAL MEDIA PAGES

Image
We desire to reach to a great audience as much as we can. We have accounts/pages in the popular social media networks particularly Facebook,instagram and our new page in twitter. All pages holds the Fasmo common theme of providing knowledge and awareness in different life subjects but mostly in Health, Nutrition and Education. We believe do as to have a great nation the citizens should be healthier and educate which will position then to be hardworkers and innovative. It is our hope our work will not be in vain but one day it will be fruitful to the local community and nation in large. Our social media pages  We use FASMO TANZANIA in all social media pages,  Facebook: Fasmo Tanzania Instagram: Fasmo Tanzania  @fasmotz Twitter: Fasmo Tanzania  @FTanzania Above all it's our lovely blog and the reader of this post you have been our great supporter. We thank you and we promise we will keep on improving day by day. Thank you and be blessed.