Posts

Showing posts from August, 2020

USTAARABU WA MEZANI (Table Manners in African Context)

Image
Ustaarabu wa Mezani (Muktadha wa Kiafrika) Table Manners (African Context) 1. Nawa mikono kabla na baada ya kula.  2. Usiongee wakati unachakula mdomoni. 3. Pakua chakula vizuri bila kudondosha pembeni 4. Wakubwa ndiyo wataanza kupakua kisha wadogo watafuata. 5. Hakikisha sehemu ya kulia chakula ni safi. (Eneo na vyombo) 6. Kaa chini kwa utulivu ndiyo uanze kula. (Usile huku unatembea, kimbia au kucheza) 7. Usiokote kilichodondoka kisha kukila. 8. Baada ya kumaliza kula safisha eneo ulilotumia kulia chakula. 9. Tafuna chakula taratibu na vizuri kabla ya kukimeza. (Huku umefunga mdomo) 10. Epuka kuongea au kusikiliza maneno yanayotia kinyaa wakati wa kula. 11. Usigongegonge chombo cha kulia (sahani/bakuli/ kikombe) chota chakula taratibu. Pia usigongegonge meza. 12. Rudisha kiti au mkeka sehemu nzuri baada ya kula. 13. Omba usogezewe kitu kilicho mezani badala ya kuamka na kukifuata (Chumvi, sukari, tunda) 14. Piga mswaki na safisha mdomo vizuri baada ya kula. ...

Mradi wa MSINGI WA LISHE BORA katika Manispaa ya MOROGORO MJINI

Image
MSINGI  WA LISHE BORA Msingi wa lishe bora ni mradi wa utoaji elimu ya lishe kwenye shule za msingi katika manispaa ya Morogoro mjini. Mradi huu umelenga kuwajengea watoto tabia na maarifa ya kujua masuala ya msingi ya lishe yatakayowasaidia kufanya maamuzi sahihi katika ulaji bora na ulaji wa afya ili kuwaepuka kupata magonjwa na matatizo ya kiafya yanayohususiana na lishe kama kisukari, matatizo ya mifupa, matatizo ya moyo, matatizo ya ini na unene uliokithiri.. Maarifa hayo ni pamoja na kujua namna nzuri za kupangilia mlo kamili kwa kujumuisha makundi yote ya chakula, kuwajengea tabia ya usafi wa chakula na mwili, kuwafumbua akili juu ya vyakula vipi wasivipe kipaumbele kwenye milo yao kutokana na wingi wa vyakula hivyo hugeuka hatari kwenye afya zetu.  Pamoja na hayo pia elimu juu ya vitu mbalimbali vya afya kama kuwafundisha ustaarabu wa mezani (table manners), mitindo mizuri ya kukaa ili kulinda afya ya mifupa na nyama pamoja na umuhimu wa Bima ya afya. Morogoro mjini...

UNYONYESHAJI NA FAIDA ZAKE

Image
UNYONYESHAJI  Wiki ya unyonyeshaji duniani ni kampeni ya dunia nzima inayoadhimishwa na nchi mbalimbali kila mwaka katika wiki ya kwanza ya mwezi wa nane (tarehe 1 hadi 7 mwezi wa nane) inayolenga kuhamasisha unyonyeshaji sahihi wa maziwa ya mama ili kuimarisha afya za Watoto. Katika mwaka 1992 ndipo wiki ya kwanza ya unyonyeshaji duniani iliadhimishwa. Kama ilivyokuwa miaka ya nyuma wiki ya kwanza ya mwezi wa nane (Agosti) kuadhimisha kwa wiki ya unyonyeshaji duniani, kauli mbiu ya mwaka huu ilikuwa“ Tuwawezeshe Wanawake Kunyonyesha Watoto kwa Afya Bora na Ulinzi wa Mazingira” . lengo likiwa ni kuwasaidia wazazi na wahudumu wa nyumbani kutoa huduma inayostahili kwa watoto tangu mama akiwa mjamzito, anapojifungua na hata baada ya kujifungua. Katika kuambatana na kauli mbinu ya mwaka huu, shirika la Afya duniani (WHO) na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto (UNICEF) wamelenga katika kushauri na kuziita serikali kuhakikisha zinalinda na kuchangia up...