USTAARABU WA MEZANI (Table Manners in African Context)
Ustaarabu wa Mezani (Muktadha wa Kiafrika)
Table Manners (African Context)
1. Nawa mikono kabla na baada ya kula.
2. Usiongee wakati unachakula mdomoni.
3. Pakua chakula vizuri bila kudondosha pembeni
4. Wakubwa ndiyo wataanza kupakua kisha wadogo watafuata.
5. Hakikisha sehemu ya kulia chakula ni safi. (Eneo na vyombo)
6. Kaa chini kwa utulivu ndiyo uanze kula. (Usile huku unatembea, kimbia au kucheza)
7. Usiokote kilichodondoka kisha kukila.
8. Baada ya kumaliza kula safisha eneo ulilotumia kulia chakula.
9. Tafuna chakula taratibu na vizuri kabla ya kukimeza. (Huku umefunga mdomo)
10. Epuka kuongea au kusikiliza maneno yanayotia kinyaa wakati wa kula.
11. Usigongegonge chombo cha kulia (sahani/bakuli/ kikombe) chota chakula taratibu. Pia usigongegonge meza.
12. Rudisha kiti au mkeka sehemu nzuri baada ya kula.
13. Omba usogezewe kitu kilicho mezani badala ya kuamka na kukifuata (Chumvi, sukari, tunda)
14. Piga mswaki na safisha mdomo vizuri baada ya kula.
15. Usikiongelee vibaya chakula mbele za watu wengine wakati wa kula.
16. Tumia mkono wa kulia wakati wa kuchota chakula.
17. Kunywa maji.
18. Shukuru kwa chakula baada ya kula. Ikiwezekana kabla na baada ya kula.
19. Endapo itakulazimu kujikuna wakati wa kula, basi tumia mkono wa kushoto au nawa kisha ujikune.
20. Kuvimbiwa ni dhambi. Kutupa chakula ni dhambi.
21. Pakua kwa kuzingatia uwiano wa walaji wengine. Usipakue chakula kingi wakati wenzako bado.
Na
Nobel Edson Sichaleh
Fasmo Tanzania.
Comments