Posts

Showing posts from 2022

Msimu wa Baridi na Afya.

Image
Kipindi cha mwezi wa sita na mwezi wa saba maeneo mengi sana ya hapa kwetu Tanzania huwa katika msimu wa baridi kali. Kuna sehemu zingine baridi huwa kali kiasi cha saruji/barafu huwepo juu ya ardhi. Baridi hufanya sisi binadamu kuwa na tabia fulani ili tupate joto na kuishi kwa amani kipindi hiki. Tunabadili mavazi kutoka mepesi kwenda mazito, mabadiliko ya muda wa kulala na muda wa kuamka. Wengine kiwango cha usafi hupungua, kutokana usafi unategemea maji kwa sana na hayo maji kipindi hiki huwa ya baridi kiasi huogopwa.  Kuna kundi la watu wao kipindi cha baridi hujikuta wanaanza kunywa pombe kali ili kuupa mwili joto bila kujali madhara ya muda mfupi na mrefu. Juu ya yote kuna tabia moja kipindi hiki cha baridi ambayo sio mbaya lakini ikikosa umakini sio salama. Tabia ya kuota moto. Moto huupasha mwili joto, wapo wanaoota kwa makundi na waoota pekeyao. Unaweza ukawa moto wa kuni au mkaa. Uotaji wa moto sio njia mbaya katika kuweka mazingira ya ujoto. Ukosefu wa umakini na kutokujua

Wanajamii Wanahitaji Elimu

Image
Jamii yetu bado inachangamoto nyingi sana. Na kwa bahati mbaya zipo changamoto ambazo zinahatarisha ubora wa kizazi kijacho kiafya na kimaadili. Jambo zuri ni kwamba wanajamii wanazijua changamoto hizo japo sio kwa upana mkubwa. Kwa mfano wanajamii wengi wanajua lishe isipokuwa nzuri inaathiri afya lakini hawajui lishe mbovu ikoje na lishe bora ikoje. Wao miaka nenda miaka rudi watajilia kile kilichopo au kile wanachopenda.  Haya twende kwenye malezi, huko nako changamoto chungu nzima. Wazazi na walezi wanajua malezi yasipokuwa mazuri yanaathiri moja kwa moja ukuaji, afya, tabia na hata masomo ya mtoto. Lakini malezi bora yamebaki kuwa changamoto kwe wengi. Usimamizi mdogo wa wazazi, mawasiliano madogo/mabaya baina ya watoto na wazazi, vipigo vikubwa, matusi na matendo mbalimbali yanayowanyima watoto haki zao za msingi.  Hatari iliyopo, matendo hayo mengi yamekuwa ndiyo mtindo wetu wa kawaida wa maisha hii inapelekea wazazi kutoambilika. Majirani nao kuchukulia kawaida au kuogopa kurip

Our New Logo

Image
Family Smile Organization, we are happy to introduce our new logo. We thank our stakeholders and friends for being with us throughout the period. The change of logo is more focused on our growth and our current and future needs. .