Tabia ya Kujisomea Vitabu.

Kujisomea vitabu kuna mfanya mtu aweze kujimudu kifikra kwa kuwa atakuwa anaishughulisha akili yake kupata mawazo mapya kutoka kwa watu wengine. Na pia atakuwa anaifikirisha akili yake kwa yale mawazo anayoyapata.


Kujisomea kuna hitaji muda na utulivu na ndiyo sabahu wengi hushindwa kuvitoa hivyo vitu kwenye maarifa. Wasoma vitabu hawasomi kwa pupa na hawasomi wakiwa hwajatulia. Utulivu huifanya akili kuweza kuunganisha mtiririko wa mawazo ambayo Mwandishi ameyawasilisha kupitia andiko lake liwe hadithi,habari, uhamasishaji na hata tungo za maisha.


Kutoa muda na kuwa mtulivu siyo vitu vya haraka kutokea, bali hujengwa katika hali ya mazoea ambayo hujenga tabia. Tabia ya kujisomea vitabu mtu hazaliwi nayo lakini huundwa na mtu au watu huambukizana. Tabia ya kupata maarifa yaliyofichwa kwenye kurasa. Tabia ya kujifunza haina mwisho maishani mwetu. Jijengee tabia ya kujisomea vitabu tena vile vitakavyokujenga kiakili,kimwili au kiroho.

Comments

Popular posts from this blog

Mitindo Yetu Ya Ulaji.

Nafasi ya Maziwa katika Afya Zetu.

MADHARA YA UTENGANO WA KIJAMII YALIYOSABABISHWA NA COVID19