Ujinga ni chanzo kikuu cha ubinafsi.

Ubinafsi ni moja ya madhara ya ujinga. Mtu kuwa na hisia kali juu yake dhidi ya wengine. Kuona yeye ndio zaidi ya wengine kwenye hilo kundi, kuhisi anastahili kupata zaidi ya wengine mfano gawio la kitu chochote, kipato hata shukurani.

Ubinafsi unaletwa na upofu wa uhalisia unaotokana na kutokujua uhalisia wa vitu au maisha na kujikuta unajiona au unajifikiria wewe tu  Ubinafsi ni ujinga.
Kutokujua pia wenzako wana thamani kama wewe, ni wahitaji kama wewe, ni watafutaji kama wewe. Ubinafsi ni kutokujua kuwa ridhiki huja kwa baraka za Mungu, kwa jitihada na kwa uwekezaji lakini wewe unachojua ni unastahili zaidi yao hata kama mpo katika daraja moja au daraja la chini yao.

Kutokana na ubora wako katika jambo fulani unaona HAKUNA KAMA WEWE!! Wakati kuna watu mnaosaidiana nao, wanaokupa mawazo na kukutia moyo. Au kuna watu ambao kama nao wangepewa nafasi kama wewe wangeweza kufanya kama wewe au hata zaidi. Kupuuzia michango ya watu wengine katika mafanikio yako na kuona ni wewe binafsi uliyejifikisha hapo ni uiinga. Jifunze kuthamini waliokuzunguka na michango yao bila kujali kiasi cha michango yao kwenye mafanikio yako.

Ubinafsi utakufanya usione makosa yako na kujihisi hukosei ila wengine ndiyo wanakosea wakati uhalisia hakuna aliyekamilika na binadamu tunaishi kwa kutegemea. Kutegemea kwamba tunahitaji kukosoana, kushauriana, kutiana moyo, na kusaidiana kwa namna tofauti. Yote haya yanahitaji uelewa wa uhalisia wa vitu(maarifa) nje ya hapo ubinafsi na chuki huzaliwa.

AMKA TAFUTA MAARIFA
#ATM2020
#Againstignorance

Comments

Popular posts from this blog

Mitindo Yetu Ya Ulaji.

Nafasi ya Maziwa katika Afya Zetu.

MADHARA YA UTENGANO WA KIJAMII YALIYOSABABISHWA NA COVID19