Siku ya Wazee Duniani
Ukiwa ni mwanzo kabisa wa mwezi wa kumi baada ya kumaliza miezi tisa ya mwaka 2020 iliyojaa mikasa mingi ya kusisimua kwenye nyanja mbalimbali za maisha hususani afya na uchumi.
Leo ni tarehe mosi ya mwezi Octoba na ni Siku ya Wazee Duniani.
JE WAJUA
❗️Kila sekunde mbili inayopita watu wawili duniani wanatimiza miaka 60? .
Mzee ni mtu mwenye busara nyingi, mlezi wa jamii na amebeba mafundisho mengi kwa kuwa ameona n kujifunza mengi katika Maisha.
Kutokana na majukumu wanayoyapitia wazee, huweza kukumbana na matatizo ya kiafya kama vile kusumbuliwa na magonjwaa kwa mfano shinikizo la juu la damu, kisukari, na maumivu ya viungo vya mwili kama vile miguu, mgongo na misuli.
Pamoja na hayo, wazee husumbuliwa na; *Msongo wa mawazo ambao mara nyingi husababishwa na kuwekwa mbali na wanafamilia, kukosa wazee wenzake wakabadilishana mawazo.
*Kukosa kipato toshelezi kuzimudu gharama za maisha na matibabu.
Katika kuadhimisha siku ya wazee dunia na
Kauli mbiu yetu inayosema:
“*Vijana tuwajibike, kuleta thamani ya wazee* ”*
Tunawashauri vijana wawasaidie wazee kutunzaa Afya zao, kwa kufuata mienendo sahihi ya Maisha:
■ Kuzingatiaa ulaji unaofaa kwa kula mlo kamili na wakutosha wenye mchanganyiko wa vyakula katika makundi 5 ya vyakula ambayo ni;
* Nafaka, mizizi na ndizi za kupikwaa.
* Vyakula venye asili ya wanyama, na jamii ya mikunde.
* Mbogamboga
* Matunda
*Na mafuta, Sukari na Asali.
KULA KWA WINGI
✅Vyakula venye wingi wa makapi lishe kama vile mbogamboga, matunda na nafaka zisizokobolewaa, kusaidi ufyozwaji wa virutubishi mwili.
✅Vyakula vyenye wingi wa vitamini na Madini kama vile samaki, maziwa, mboga na matundaa kuimarisha kingaa ya mwili dhidi ya mangonjwa.
✅Vyakula venye kiasi kidogo cha nishati lishe kama vile sukari, mafuta na Chumvi, kujikinga dhidi ya magonjwa yasioambukizwa kama vile shinikizo la juu la damu na kisukari.
✅Vyakula venye asili ya wanyama na jamii ya mikunde, kujengaa mwili na kuimarisha mifupa na misuli.
✅ Kula milo midogomidogo kama vile juisi asili ya matunda na matunda, ili kujengaa mwili.
Haitoshi kufuata ulaji unaofaaa pekee, hivyo tunashauri
✅Ufanyaji wa shughuli mbalimbali ili mwili usibweteke ukawa rahisi kushambuliwa na magonjwa. Shughuli kama kutembea, kukimbia, kufua nguo hata shughuli za bustani pia.
✅kuzingatia usafi wa mwili, mavazi na mahali pa Kuishi.
✅ kujenga tabia ya kupima Afya mara kwa mara kwa Afya bora.
✅Kuachaa uvutaji wa sigara, ugoro na tumbaku na unywaji wa pombe.
Kama ilivyo kauli mbiu ya mwaka kuu kuwa "Familia na Wazee tuwajibike, kuwatunzaa wazee"
Ni muhimu vijana kuwa jibika na kuwatunzaa wazee wetu.
Kwa chochote tulichojaaliwa basi tukitumie na kukiwekezaa kwa wazee wetu kwa: ✅Kuwaheshimu wazee.
✅Kuwasaidia kupata chakula, kuboresha makazi ya wazee, kuhudumia afya zao.
✅Kutambuaa fursa walizonazo na kuwasaidiaa kufikia malengo yao ili waweze kuweza kupata kipato kinachokizi mahitaji yao na kuepukana kuwa tengemezi..
Pamoja na mambo mengine mengi ndiyo yataongeza thamani za wazee na sio kuwatelekeza kuwaacha wapweke.
Juu ya yote tunatoa pokezi kwa taasisi za Kiserikali na binafsi pamoja na vituo vya kulelea Wazee, katika kuwasaidia wazee kupata mahitaji yao.
Hivyo tunapendekezaa, kuwepo na msaada na nguvu kuweza kuziwezesha taasisi mbalimbali za serikali, binafsi na dini ziwaangalie wazee kwa jicho lingine;
✅kuongeza idadi ya nyumba za kuwatunza wazee. Kuna wazee wengi wenye uhitaji hapa nchini kwetu kwa kuwa wengi hawakubahatika kupata kazi wakati wa ujana wao hivyo hawana mafao au kiinua mgongo chochote, na katika hekaheka za maisha wengine walipata ulemavu, wengine walifiwa na vijana wao hivyo wamejikuta ombaomba ili kupata mahitaji yao.
✅Kujengaa ushirikiano miongoni wa taasisi mbalimbali zinazowasaidia wazee ili kuongezaa nguvu zaidi kuwasaidia wazee.
✅Kutoa fursa mbali mbali za Maendeleo kama vile kilimo na ujasiriamali kwa wazee, ili kuwainua wazee kiuchumi.
*KWA PAMOJA TUJENGE TAIFA LA WAZEE IMARA💪*
Na
Rahma Sheshe
Mtaalamu wa Lishe na jamii
Fasmo Tanzania & WazeeHub
Comments