SIKU YA CHAKULA DUNIANI
Tarehe 16 mwezi oktoba kila mwaka ni maadhimisho ya Siku ya chakula duniani. Siku hii ilihasisiwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Kilimo na Chakula, (FAO) mnamo mwaka 1979. Tarehe ya leo pia ni maadhimisho ya miaka 75 ya FAO tangu kuanzishwa kwake. Lengo kuu la maadhimisho haya ni kuongeza uelewa kwa watu kuhusu umuhimu wa chakula na uhakika wa chakula na lishe kwa watu wote duniani hasa wale walio katika hatari ya kukosa chakula kabisa. Chakula ni moja kati ya mahitaji muhimu ya kila binadamu, hivyo ni sehemu ya maisha yetu kila siku kwa kuwa bila chakula uhai wetu hutetereka. Hivyo, tunaposherehekea siku ya chakula duniani, jiulize; 1. Nina uhakika wa chakula? Kama ndiyo (naweza kununua, kuandaa na kula chakula cha kutosha) je vipi kuhusu ambao hawawezi kula hata mlo mmoja kwa siku? 2. Chakula ninachokula ni salama? Ni kisafi, kimeandaliwa katika hali gani, hakina vijidudu vyovyote au sumu ya aina yoyote itokanayo na vijidudu hivyo (kama vile sumukuvu itokanayo na kuvu ...