NILISHE NIFAULU

NILISHE NIFAULU
Ni mradi unaotekelezwa na asasi isiyokuwa ya kiserikali ya FASMO ikishirikiana na wanajamii. Mradi huu umelenga utoaji wa chakula katika shule za msingi kama njia kuu ya kuchochea mahudhurio na utulivu wakati wa kujifunza ambavyo kwa pamoja huchangia matokeo bora (ufaulu) kwa wanafunzi na shule kwa ujumla.
Familia nyingi za Kitanzania zina uwezo mdogo wa kiuchumi. Watoto hulazimika kuamka asubuhi sana na kukimbilia shule bila kupata kitu chochote cha kula. Na kwa bahati mbaya hata shuleni hakuna utaratibu wa ugawaji wa chakula hivyo mtoto hujikuta masaa zaidi ya saba hajapata chakula kwa kuwa hata hela ya matumizi shuleni hajapewa au ni ndogo sana. 
Uelewa wa wanafunzi huwa hafifu kutokana na mazingira hayo ya ukosefu wa chakula wakati wa masomo. Pia ukosefu wa chakula huchochea sana utoro na wanafunzi kuacha shule. 
Utoro katika sura mbili, sura ya kwanza wanafunzi kutokuja shule na sura ya pili mwanafunzi au wanafunzi kutohudhuria kipindi au vipindi, hii ni pale mwanafunzi kaja shule lakini anaondoka shuleni bila ruhusa na sababu ya msingi. Na sababu mojawapo inayowafanya watoroke shule ni njaa.
 Ushahidi wa kimazingira kutoka sehemu mbalimbali haswa katika shule ambazo zinahuduma ya chakula mahudhurio yapo juu na utoro umepungua mno kuringalisha na shule ambazo hazina huduma ya chakula.

Kwa nini Nilishe Nifaulu
Kuna mrundikano wa sababu mbalimbali zilizochochea kubuniwa kwa mradi huu, sababu hizo ni ...
●Kuchochea ufaulu wa wanafunzi kitaaluma.
●Kuboresha hali za afya na lishe kwa wanafunzi.
●Kuchochea mahudhurio na kupunguza utoro.
●Kuokoa muda ambao ungetumiwa na wanafunzi kurudi majumbani kwao kula chakula kisha kurudi shule na kuendelea na masomo.
●Kusaidia watoto wanaotoka katika mazingira magumu yanayochangia kukosa hela ya matumizi shuleni na kujikuta wanashinda njaa au kuwadoea wengine.
●Kuchochea mshikamano kati ya wazazi na shule. Uwepo wa mradi kama huu unachochea ukaribu wa pande hizi mbili muhimu katika maendeleo ya mtoto kitaaluma na kimalezi.

Ni muhimu sana huduma za chakula katika shule za msingi kwa kuwa ndiyo wakati wa ukuaji wa ubongo na tabia kama umakini utatumika katika kusaidia ukuaji mzuri basi mtoto atakua na kufanikiwa kwenye vitu vingi kwa kuwa msingi wa malezi ulikuwa bora. Hii ndiyo sababu iliyotuchochea kuja na mradi huu.
Mradi huu kwa sasa unahudumia shule ya msingi Kilakala iliyopo manispaa ya Morogoro. Mradi ulianza mwezi Oktoba  2020 na umeonyesha mafanikio kadha wa kadha hususani kuongezeka kwa uchangmfu wa wanafunzi kwenye vipindi baada ya mapumziko jambo ambalo halikuwepo kabla ya huduma hii kuanzishwa shuleni hapo. 
Tunatarijia kuuboresha na kuutanua mrafi huu kufikia wanafunzi wengi hapa Tanzania wanaotoka katika mazingira magumu kama vile umaskini, umbali na shule, maeneo yenye lishe duni na ufaulu duni. Lengo kuu ni kuijenga kesho bora kwa kuwatemgenezea mazingira bora ya elimu. Maboresho mengi yatahusu ujumuishwaji wa jamii katika mradi.
Jamii ya Kitanzania ina kila sababu ya kuunga juhudi hizi kuwawezesha watoto kupata elimu bora katika mazingira rafiki.

NILISHE NIFAULU!

Comments

Anonymous said…
Mambo si ndiyo haya. Kazi njema

Popular posts from this blog

Mitindo Yetu Ya Ulaji.

Nafasi ya Maziwa katika Afya Zetu.

MADHARA YA UTENGANO WA KIJAMII YALIYOSABABISHWA NA COVID19