Posts

MAJI NA AFYA ZETU

Image
Maji ni afya, maji ni kinga. Kuna faida lukuki kwa unywaji wa maji. Je wajua sehemu kubwa ya mwili wa binadamu imetengenezwa kwa maji, kwa maana kwamba viungo na tishu mbalimbali mwilini vimeundwa kuhusisha maji..kwa mfano damu, misuli na hata mafuta mwilini yana maji kwa kiasi chake pia. Karibu asilimia 60 hadi 75 uzito wa mwili wa binadamu ni maji ingawa kunakuwa na tofauti za kiasi cha maji kulingana na jinsia, umri, mazingira, aina za shughuli mtu anafanya nakadhalika Dalili zinazoonesha mtu kapungukiwa maji mwilini 1. Harufu mbaya ya kinywa  2. Ngozi kuwa kavu 3. Maumivu ya kichwa (ingawa sio kila maumivu ya kichwa ni upungufu wa maji) 4. Kizunguzungu (ingawa sio kila hisia za kizunguzungu husababishwa na upungufu wa maji mwilini) 5. Uchovu wa mwili 6. Midomo kuwa mikavu (watu wengi huonesha dalili hii na huonekana sehemu ya nje ya midomo - lips) 7. Kutopata choo mara kwa mara au kupata choo kigumu na kwa shida (constipation) Kuna baadhi ya dalili hapo ...

MADHARA YA UTENGANO WA KIJAMII YALIYOSABABISHWA NA COVID19

Image
Madhara ya Utengano wa Kijamii yaliyoletwa na COVID19 Nchi nyingi sasa duniani zimeanza kulegeza masharti ya tahadhari zilizowekwa zifuatwe ili kupunguza na hata kutokomeza maambukizi na madhara ya janga la virusi vya Korona. Ugonjwa wa Korona umeleta madhara mengi ya muda mfupi na mengine ya muda mrefu. Itachukuwa muda jamii yetu kurudi kwenye maisha ya kawaida, kiuchumi na kimahusiano baina ya watu hili ni kutokana na tahadhari tunazochukua na tulizochukua katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Covid19. Leo naomba tuzungumzie madhara ya muda mfupi na muda mrefu ya Kujitenga kijamii (Social distancing/Isolation ). Kujitenga kijamii ni moja ya njia iliyobuniwa na kuhamasishwa itumike katika kuzuia maambukizi ya Corona. Njia hii ililenga mtu kukaa umbali wa Mita moja na zaidi na hata kujifungia ikiaminika umbali huo mtu aongeapo au akikohoa virusi haviwezi kumfikia mwingine kwenye huo umbali. Njia hii imekuwa na msaada kwa kupunguza kasi ya maambukizi ndani ya wanajamii kwenye...

Shairi: LISHE NAISHIKIA KIPAZA

Image
LISHE NAISHIKIA KIPAZA Leo jukwaani najongea, Sauti yangu kuipaza, Kuna kitu nataka kuongea, Muda sasa cha nikwaza, Wasio na sauti wataponea, Rafiki yao nashika kipaza. Ni kwa muda sasa, Jamii yetu ii taabani, Lishe yaonekana anasa, Wakulaumiwa nani? Viongozi wa kisiasa, Au mitaala ya kizamani? Tunazalisha mazao, Hatujui kuyatumia, Watu wala kikwao, Vyakula hufakamia, Shida huja afya zao, Gharama kujitibia. Laiti ingetolewa elimu, Mitaani na darasani, Wangejua umuhimu, Nini kiwepo kwa sahani, Magonjwa wangekuwa adimu, Ukosefu wa vyakula fulani. Bungeni ingekuwepo kamati, Yenye uongozi makini, Iliyojaa mipango mikakati, Kuwafikia watu wa chini, Na kuwawezesha kwa dhati, Elimu ya lishe waushinde umaskini. Lishe kwa mtoto na mama, Ila sio kwa wao tu aisee, Lishe ni jambo la maana, Kwa vijana pia wazee, Wote tuseme hapana, Kula mlo mmoja pekee. Mkulima ukitoka kuvuna, Mavuno hifadhi vizuri, Pindi yatapokuwa hakuna, Ghala lako lisiwe sifuri, Utaendelea kutafuna, Ukifanya zingine shughuli. K...

COVID19 na Vitamini D

Image
Habari za saa hizi mpendwa msomaji wa makala zetu!  Ni matumaini yetu unaendelea vizuri kiafya na upo wima katika mapambano dhidi ya Corona kwa kuchukuwa tahadhari zote muhimu kujilinda na kuwalinda waliokunzunguka msipate maambukizi. Leo tutaongelea juu ya Vitamini D dhidi ya Corona. Hadi sasa kuna tafiti nyingi kuhusu ugonjwa huu wa Covid 19 zimefanyika na zinaendelea kufanyika na tafiti hizi hutofautiana hasa katika kuhusianisha ugonjwa huu na vitu kadha wa kadha. Ingawa CHAKULA (Lishe na Virutubishi) ni moja kati ya vitu ambavyo vimekuwa vikizungumziwa na kufanyiwa utafiti kwa kiasi kikubwa sehemu mbalimbali ulimwenguni tangu mlipuko wa ugonjwa huu uanze disemba 2019 huko China.. Hapa kwetu Tanzania kumekuwa na msisitizo mkubwa kutoka kwa wataalamu wa afya na lishe kuhusu ulaji wa Vyakula vyenye Vitamini C kwa wingi kama vile malimao, machungwa, tangawizi, mananasi, vitunguu swaumu, ndimu, mboga za majani kama vile giligilani, bila kusahau mapera (yaliyosahaulika na...

NAMNA VIRUSI VYA CORONA VINAVYOSABABISHA COVID19 HUPIMWA

Image
NAMNA VIRUSI VYA CORONA VINAVYOSABABISHA COVID19 HUPIMWA Mpaka sasa kuna vipimo (vitendanishi) vya aina kuu mbili vinavyotumika kupima covid-19 vinavyotumika sehemu nyingi duniani kutambua watu wenye maamumbikizi ya ugonjwa huu wa mlipuko uliosambaa sehemu karibu zote za dunia. Aina ya kwanza ni kile kinacho pima covid-19 kwa kuangalia uwepo wa kinasaba cha kirusi chenyewe (RNA). Kipimo hiki hujulikana kama ‘Real-time Reverse Transcription Polymerase Chain Reaction’ (RT-qPCR) au al-maarufu PCR! Hiki ndio kipimo mashuhuri na ‘standard’ kinachotumika ulimwenguni kwa sasa. Sampuli zake huchukuliwa kwa kulambisha (swab) kijiti cha pamba (cotton swab) ndani-nyuma ya pua (nasophyaryngeal swab) na/au ndani-nyuma ya mdomo (oropharyngeal swab). Aina ya pili ni ile inayopima kwa kuangalia kinga (antibody) inayozalishwa na muathirika pindi anapopata maambukizi ya kirusi cha corona. Kipimo hichi hujulikana kama ‘Immune Rapid Test, na vipo vya aina tofauti. Aina ...

Huduma ya Kangaroo Katika Malezi ya Mtoto

Image
Huduma ya Kangaroo katika malezi ya mtoto Mgusano wa ngozi kwa ngozi kati ya mzazi na mtoto maarufu kwa jina la  "Huduma ya Kangaroo" ni huduma ambayo wazazi hususani akina mama huwapa watoto wao kipindi wakiwa wachanga. Huduma hii inafaida kubwa kwa watoto na kwa wazazi pia, kwa kuwa inaongeza ukaribu kati yao. Huduma ya Kangaroo Maneno "huduma ya kangaroo" ilikuwa inaitwa kwa kufanana kwake na jinsi Kangaroo hubeba watoto wao. Huduma ya ngozi kwa ngozi huiga mazingira ya kinga na ya uleaji ya mfuko wa kangaroo. Kwa ufafanuzi, utunzaji wa kangaroo ni utunzaji wa maendeleo kwa kugusanisha ngozi ya watoto wachanga dhidi ya kifua cha mama au baba. Huduma ya kangaroo ilianza katika miaka ya 1970, kama njia ya kukuza utunzaji na kunyonyesha mapema kwa watoto wachanga wa waliozaliwa ndani wa muda. Mwishoni mwa 1970, shughuli hii ilipanuliwa kwa watoto wachanga waliozaliwa kabla ya miezi tisa kutokana na viwango vya vifo vingi, viwango vya juu vya maam...

HAKI ZA MGONJWA POPOTE PALE

Image
HAKI ZA MGONJWA Katika maisha kwa sababu  mbalimbali mwanadamu hupatwa na udhaifu wa mwili hivyo hujikuta akitafuta tiba kwenye taasisi za kutolea tiba za afya. Taasisi hizo hutoa huduma mbalimbali na katika kupokea huduma mgonjwa huwa na haki zifuatazo ● Haki ya kusikilizwa ●Mgonjwa ana haki ya kujua huduma za afya zinazotolewa katika hospitali, ikiwa ni pamoja na mkalimani endapo mgonjwa haimudu lugha ya kawaida katika eneo hilo. ●Haki ya kutaka gonjwa lake liwe siri ●Haki ya kuulizia na kuambiwa majibu ya vipimo vyake ●Haki ya kukataa kuendelea na matibabu ●Haki ya kuomba abadilishiwe mtalaamu (Daktari/Muuguzi) ● Mgonjwa ana haki ya kujua ni nani anayetoa huduma za matibabu na ni nani anayehusika na kumuhudumia.. ●Haki ya kupewa elimu ya kujikinga au kujiepusha na magonjwa ●Haki ya kupewa ufafanuzi toshelezi juu ya matumizi ya dawa ●Haki ya kupewa ufafanuzi wa gharama za matibabu yake ●Haki ya kuhudumiwa kama wagonjwa wengine bila ...