Posts

Showing posts from 2021

Shinikizo Kubwa la Damu

Image
 SHINIKIZO KUBWA LA DAMU  Utangulizi  Moyo unapopiga, husukuma damu kwenye mishipa ya damu ili isambae mwilini kote.  Shinikizo la damu ni hali ambapo msukumo huu wa damu unazidi kiwango cha kawaida na unaweza kusababisha madhara mwilini.  Madhara ya shinikizo kubwa la damu Shinikizo kubwa la damu linaweza kuleta madhara mbalimbali yakiwemo: • Kupasuka kwa mishipa ya damu kichwani na kusababisha kuharusi. Kiharusi ni moja ya sababu kubwa za vifo vya watu wazima  • Moyo kupanuka na hatimaye kushindwa kufanya kazi yake ya kusukuma damu.  • Kuharibika kwa mishipa ya damu kwenye figo na hatimaye figo kushindwa kufanya kazi yake ya kusafisha damu.  • Mishipa mikubwa ya damu kuharibika kwa sababu ya kuvuja kwa virutubishi vilivyo kwenye damu na kusababisha kiharusi, ugonjwa wa moyo au miguu kutopata damu ya kutosha.  Dalili ya shinikizo kubwa la damu  Wengi wa watu wenye shinikizo kubwa la damu hawana dalili zozote. Waliobaki wanaweza kuwa na dalili zifuatazo:  • Kuumwa kichwa mara kwa mara....

Yakimbie Magonjwa Sugu Yasiyoambukizwa.

Image
Tupo ndani ya mwezi wa kuadhimisha kujikinga na kupambana na magonjwa sugu yasiyoambukiza. Maadhimisho haya haswa huanza tarehe 6 hadi 13 mwezi Novemba kila mwaka ambapo hiyo wiki huwa ni kilele chake.  Lengo la maadhimisho haya ni kuifahamisha na kukumbusha jamii uwepo wa magonjwa haya hatari na kujua jinsi ya kujikinga na kuyatibu. Magonjwa yasiyoambukiza ni magonjwa yote ambayo hayawezi kuambukizwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine. Mara nyingi huwa ni ya kudumu na ni matokeo ya muunganiko wa sababu za kijenetiki, mazingira, tabia pamoja na fiziolojia (ufanyaji kazi wa sehemu mbalimbali za mwili wa mtu).  Mfano wa magonjwa haya ni kama magonjwa ya mfumo wa mzunguko wa damu (kiharusi na mshtuko wa moyo), kisukari, saratani na magonjwa katika mfumo wa upumuaji kama vile athma (asthma). Magonjwa mengine ni kama magonjwa ya akili, majeraha, selimundu na ulemavu.  Kati ya magonjwa haya, magonjwa katika mfumo wa mzunguko wa damu yanaongoza kusababisha vifo vya watu wengi zaidi dun...

Sisi na Elimu Yetu

Image
Nikiwa kwenye hekaheka za maisha nilijikuta nimetokea kwenye kijiwe kimoja cha magazeti. Kijiwe hiki sio kigeni kwangu kwa kuwa nimekuwa najituliza hapo mara kwa mara na kushiriki nao mijadala mbalimbali ya kijamii na iliyopamba vichwa vya habari vya magazeti. Kutokana na kijiwe hiki kuwa na biashara ndani yake basi watu wa rika na jinsia tofauti huja kununua magazeti na kupiga soga huku wauza kahawa nao wakishinda hapo kusukuma gurudumu. Kijiwe hiki kina sheria mbili kuu, mosi huruhusiwi kutumia lugha ya matusi eneo hilo. Pili ni marufuku kuvuta sigara eneo hilo. Ni sheria hizi mbili zinazofanya wengi kutonunua magazeti na kuondoka kwa haraka, huvuta muda kujadili kitu kidogo kwa kuwa staha ni kubwa. Nikiwa kijiweni watu wote wanachangia maada ambayo pia imetawala mitandaoni. Mada yenyewe ni "Elimu Itolewayo Tanzania na Mustakabali Wake". Kijiwe hiki kama vilivyo vijiwe vingi hapa mjini, watu wanajua sana vitu. Watu wanaupeo na upendo inapokuja suala la kuandaa hatma nzuri y...

FURAHIA UNENE AU UPUNGUZE KWA STAHA

Image
Watu wengi huanza taratibu za kupunguza uzito wa mwili sababu tu wameambiwa ' aise umenenepa ' na mtu fulani au kwa sababu amevutiwa na mwenzie ambaye mwili wake ni mdogo au kuona nguo nyingi zimeshaanza kuwa ndogo au kwa sababu kasikia unene au uzito uliozidi sio salama kiafya.  Ila ukweli ni kwamba, hata kama utaweza kuyafikia malengo ya kupunguza unene/uzito wa mwili wako ni kheri kuyafikia malengo yako kwa njia sahihi ambayo itakuwezesha kudumisha uzito wa mwili wako bila kuumiza wala kukuletea madhara mwilini. NIJUE NINI KABLA YA KUANZA KUPUNGUZA UZITO WA MWILI? Ni vyema kufahamu ya kuwa kuwa na uzito uliozidi sio dhambi ingawa watu wengi hutumia muonekano wa watu wanene (ambao mara nyingi huwa na uzito uliozidi) kuwatania kwa kuwaita majina mabaya na unyanyapaa mwingine na kwa kiasi kikubwa hii ikimpata mtu ambaye hajikubali jinsi alivyo, basi hupelekea kufanya vitu vyenye madhara zaidi. 1. Tambua ya kuwa uzito wa mwili huchangiwa na sehemu kubwa mbili, sehemu...

FAHAMU KUHUSU UZITO WAKO

Image
Watu wengi hufikiria uzito uliozidi mwilini ni wingi wa mafuta tu. Kwa upande mmoja fikra hizi huchangiwa na kile wanachokiona kwa mtu husika, yaani mtu kuonekana akiwa na amejaa nyama uzembe mfano upande wa mbele wa tumbo/ kitambi (haswa wanaume ingawa siku hizi hata wanawake wanakuwa na vitambi pia) au sehemu zingine za mwili mapajani, kiunoni na kifuani.  Maana ya uzito wa mwili. Uzito wa mwili huchangiwa na mafuta, misuli, mifupa, tishu zingine zikiwa na maji au ni sawa na kusema uzito wa mtu upo katika sehemu kuu mbili, yaani uzito wenye mafuta (fat mass) na ule usiohusisha mafuta (fat free mass). Unaposema mtu ana kilogramu 50, maana yake uzito huu umechangiwa na vitu vyote vilivyotajwa hapo juu bila kuhusisha nguo wala kitu kingine chochote. Na msemo kwamba takribani 75% ya mwili wa binadamu ni maji maana yake ni kwamba asilimia hizi zinachukua sehemu yote ya uzito wa mtu, yaani asilimia zinazobaki ndio uzito halisi wa kila kinachobaki mwilini baada ya kutolewa maji ...

Shairi: IWE LEO

Image
IWE LEO Naomba iwe leo, Kesho mbona mbali? Tuwaongeze upeo, Wakulima kila mahali, Wapate maendeleo, Kwa sera za serikali. Furahisha wakaribu, Wambali watasogea, Serikali inayo sababu, Wakulima kutetea, Miaka wapata tabu, Hayupo kuwasemea. Bajetiye iwe nono, Wafikiwe vijijini, Wapanuliwe maono, Wasilime kizamani, Waachie la mkono, Wahifadhi ghalani. Jicho umwagiliaji, Sayansi shambani, Wapate mengi maji, Wasingoje mvuani, Waongeze uzalishaji, Tuwauzie majirani. Kilimo kipae thamani, Nao wakwae ukwasi, Walioko shambani, Waendelee kwa kasi, Wote wa masokoni, Uchumi wajinafasi. Miundombinu mazingira, Isiyotegemea misimu, Wapewe malengo dira, Vikundi wapate elimu, Kilimo kifanyike ajira, Kisiishie kuwakimu. Kweli kesho nayo siku, Lakini leo yawezekana, Tupitishe sera sumaku, Kilimo kiwavutie vijana, Wengi wakimbilie huku, Kilimo kiwe cha maana. Paza Sauti Wakulima Wanyanyuke Kiuchumi, Kiteknolojia na Kiuzalishaji. Imeandaliwa na, Nobel E Sichaleh. 0783961...

Misemo na Methali Zenye Uchakula

Image
Kwenye maisha yetu ya kila siku tunaishi tuzizungumza. Tunazungumza kwa kutumia lugha yetu adhimu kabisa ya kiswahili huku tukiongelea vitu mbalimbali kwa lugha ya kawaida, lugha ya kimazingira na lugha ya kufikirika ili kufanikisha mawasiliano baina yetu. Katika maongezi yetu misemo na methali hutumika kwa sana katika kuwasiliana hii ni pamoja na kuonyana, kuhamasishana, kufarijiana na kuburudishana.  Leo ikiwa ni siku nzuri kabisa nimeona vyema tufurahi pamoja kwa kukumbushana methali na misemo tunayoitumia kila siku kwenye jamii yetu lakini ina taswira yenye uchakula yani yenye imeelezea mazingira ya ulaji kama vile chakula, kinywaji, shamba au utafutaji. 1. Kuvunjika kwa mwiko sio mwisho wa kupika. 2. Chovya chovya humaliza buyu la asali. 3. Ukimchunguza sana bata hutomla. 4. Kipenda roho hula nyama mbichi. 5. Kikulacho kinguoni mwako. 6. Mwenye shibe hamkumbuki mwenye njaa. 7. Shibe mwana malevya, njaa mwana malegeza. 8. Kizuri kula na nduguzo. 9. Mbuyu ulianza kam...

Je Mazingira ya Shule nchini yanachukua tahadhari kuwalinda watoto na magonjwa?

Image
Dunia ikiwa bado ikipambana na janga la Korona na nchi nyingi zikiwapatia wananchi wake chanjo na kulegeza sheria za tahadhari za kupambana na gonjwa hilo ambalo linaambukizwa kwa njia ya hewa. Baadhi ya nchi ziliwahi sana kuruhusu shughuli za masomo kwa wanafunzi wa shule za msingi hadi chuo huku zikitoa masharti ya kuzingatiwa wakati wa masomo.  Moja ya nchi hizo ni Tanzania, bila kutazama sana jinsi nchi yetu ilivyopambana na janga la Korona makala hii fupi imejikita katika kuangalia kwa makini mazingira ya shule hususani za msingi na sekondari jinsi yanavyoweza kulinda afya za wanafunzi au kuchochea maambuzi ya magonjwa mbalimbali yenye mfanano wa namna ya kuambukizwa na kukumba watu wengi.  Mazingira ya usafi wa madarasa, vyoo vya wanafunzi, uwepo wa maji tiririka ya kunawa na usafi kwa jumla kwa shule nyingi za msingi za serikali bado ni kitendawili. Hii kwa shule zote bila kujali eneo iliyopo, shule zilizopo mjini zina changamoto zake lukuki ikiwemo mazingira ya uuza...