Posts

Siku ya Maziwa Duniani. Tusherekee au Tusimame na Kujitafakari?

Image
MAZIWA MAZIWA MAZIWA! Tulipokuwa shuleni tulijifunza makundi ya Wanyama kulingana na sifa zao. Moja ya kundi hili ni mamalia ambao sifa yao kuu ni Wanyama wanaonyonyesha akiwemo popo, binadamu, mbwa, ng’ombe, mbuzi, kondoo nk. Wanyama hawa hufanya hivi kwa kipindi Fulani na kuacha kunyonyesha mtoto/watoto wao. Kwa mfano, ndama wa ng’ombe haachishwa akiwa na umri wa miezi 4 hadi 5, baadhi ya jamii za nyani huendelea kunyonyesha watoto wao hadi wanapofikia umri wa miaka 4 wakati tembo huendelea kumnyonyesha mtoto wake hata akiwa na umri wa Zaidi ya miaka 2. Hii ina maanisha kila mnyama anaezalisha maziwa ni kwa ajili ya mtoto/watoto wake tu. Pia tutakubali kuwa kila mnyama ana tabia zake katika kumuachisha mtoto wake kunyonya. Kwa binadamu, inashauriwa mtoto anyonyeshwe hadi atakapotimiza umri wa miaka 2 na ikiwezekana aendelee kunyonyeshwa, ingawa watu wengi hawafanyi hivyo. Wengine huishia mwaka mmoja na nusu na kuacha kumnyonyesha mtoto wake. Leo ni kilele cha maadh...

Mfumo wetu wa mmeng’enyo wa chakula, je umesahaulika?

Image
Mfumo wetu wa mmeng’enyo wa chakula, je umesahaulika? Ukikaa ukaangalia mambo mengi kwa makini utaona kwamba watu wengi huangaika na uzuri wa sehemu za miili yao wanazoziona. Ndio maana utakuta kuna huduma nyingi sana zinazohusu kutengeneza kucha, nywele (almaarufu kama saluni), kufanya maseji ya sehemu mbalimbali za mwili, skrabu. Ingawa huduma za afya zipo maeneo mengi lakini huduma ya uchunguzi ya mfumo wa chakula haipewi kipaumbele kama sehemu kubwa ya inayoweza kutumika kutatua matatizo mengi ya afya yanayoisibu jamii. Ni mara chache sana watu wengi wakipatwa na shida za kiafya hufikilia kuhusu afya ya mfumo wa mmeng’enyo wa chakula. Hii sio kibongo bongo tu bali hata nchi za wenzetu suala hili halipewi kipaumbele na watu wa kawaida pamoja na wale walioelimika katika sekta ya afya (wataalamu wa lishe, madaktari, wafamasia n.k) Hii ina maana kwamba kuna uwezekano mkubwa, matatizo mengi ya afya zetu yanaweza yakawa yanatokana na shida zilizopo katika mfumo huu kwa unafanya kazi kubw...

Msimu wa Baridi na Afya.

Image
Kipindi cha mwezi wa sita na mwezi wa saba maeneo mengi sana ya hapa kwetu Tanzania huwa katika msimu wa baridi kali. Kuna sehemu zingine baridi huwa kali kiasi cha saruji/barafu huwepo juu ya ardhi. Baridi hufanya sisi binadamu kuwa na tabia fulani ili tupate joto na kuishi kwa amani kipindi hiki. Tunabadili mavazi kutoka mepesi kwenda mazito, mabadiliko ya muda wa kulala na muda wa kuamka. Wengine kiwango cha usafi hupungua, kutokana usafi unategemea maji kwa sana na hayo maji kipindi hiki huwa ya baridi kiasi huogopwa.  Kuna kundi la watu wao kipindi cha baridi hujikuta wanaanza kunywa pombe kali ili kuupa mwili joto bila kujali madhara ya muda mfupi na mrefu. Juu ya yote kuna tabia moja kipindi hiki cha baridi ambayo sio mbaya lakini ikikosa umakini sio salama. Tabia ya kuota moto. Moto huupasha mwili joto, wapo wanaoota kwa makundi na waoota pekeyao. Unaweza ukawa moto wa kuni au mkaa. Uotaji wa moto sio njia mbaya katika kuweka mazingira ya ujoto. Ukosefu wa umakini na kutokujua ...

Wanajamii Wanahitaji Elimu

Image
Jamii yetu bado inachangamoto nyingi sana. Na kwa bahati mbaya zipo changamoto ambazo zinahatarisha ubora wa kizazi kijacho kiafya na kimaadili. Jambo zuri ni kwamba wanajamii wanazijua changamoto hizo japo sio kwa upana mkubwa. Kwa mfano wanajamii wengi wanajua lishe isipokuwa nzuri inaathiri afya lakini hawajui lishe mbovu ikoje na lishe bora ikoje. Wao miaka nenda miaka rudi watajilia kile kilichopo au kile wanachopenda.  Haya twende kwenye malezi, huko nako changamoto chungu nzima. Wazazi na walezi wanajua malezi yasipokuwa mazuri yanaathiri moja kwa moja ukuaji, afya, tabia na hata masomo ya mtoto. Lakini malezi bora yamebaki kuwa changamoto kwe wengi. Usimamizi mdogo wa wazazi, mawasiliano madogo/mabaya baina ya watoto na wazazi, vipigo vikubwa, matusi na matendo mbalimbali yanayowanyima watoto haki zao za msingi.  Hatari iliyopo, matendo hayo mengi yamekuwa ndiyo mtindo wetu wa kawaida wa maisha hii inapelekea wazazi kutoambilika. Majirani nao kuchukulia kawaida au kuogopa kurip...

Our New Logo

Image
Family Smile Organization, we are happy to introduce our new logo. We thank our stakeholders and friends for being with us throughout the period. The change of logo is more focused on our growth and our current and future needs. .

Shinikizo Kubwa la Damu

Image
 SHINIKIZO KUBWA LA DAMU  Utangulizi  Moyo unapopiga, husukuma damu kwenye mishipa ya damu ili isambae mwilini kote.  Shinikizo la damu ni hali ambapo msukumo huu wa damu unazidi kiwango cha kawaida na unaweza kusababisha madhara mwilini.  Madhara ya shinikizo kubwa la damu Shinikizo kubwa la damu linaweza kuleta madhara mbalimbali yakiwemo: • Kupasuka kwa mishipa ya damu kichwani na kusababisha kuharusi. Kiharusi ni moja ya sababu kubwa za vifo vya watu wazima  • Moyo kupanuka na hatimaye kushindwa kufanya kazi yake ya kusukuma damu.  • Kuharibika kwa mishipa ya damu kwenye figo na hatimaye figo kushindwa kufanya kazi yake ya kusafisha damu.  • Mishipa mikubwa ya damu kuharibika kwa sababu ya kuvuja kwa virutubishi vilivyo kwenye damu na kusababisha kiharusi, ugonjwa wa moyo au miguu kutopata damu ya kutosha.  Dalili ya shinikizo kubwa la damu  Wengi wa watu wenye shinikizo kubwa la damu hawana dalili zozote. Waliobaki wanaweza kuwa na dalili zifuatazo:  • Kuumwa kichwa mara kwa mara....

Yakimbie Magonjwa Sugu Yasiyoambukizwa.

Image
Tupo ndani ya mwezi wa kuadhimisha kujikinga na kupambana na magonjwa sugu yasiyoambukiza. Maadhimisho haya haswa huanza tarehe 6 hadi 13 mwezi Novemba kila mwaka ambapo hiyo wiki huwa ni kilele chake.  Lengo la maadhimisho haya ni kuifahamisha na kukumbusha jamii uwepo wa magonjwa haya hatari na kujua jinsi ya kujikinga na kuyatibu. Magonjwa yasiyoambukiza ni magonjwa yote ambayo hayawezi kuambukizwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine. Mara nyingi huwa ni ya kudumu na ni matokeo ya muunganiko wa sababu za kijenetiki, mazingira, tabia pamoja na fiziolojia (ufanyaji kazi wa sehemu mbalimbali za mwili wa mtu).  Mfano wa magonjwa haya ni kama magonjwa ya mfumo wa mzunguko wa damu (kiharusi na mshtuko wa moyo), kisukari, saratani na magonjwa katika mfumo wa upumuaji kama vile athma (asthma). Magonjwa mengine ni kama magonjwa ya akili, majeraha, selimundu na ulemavu.  Kati ya magonjwa haya, magonjwa katika mfumo wa mzunguko wa damu yanaongoza kusababisha vifo vya watu wengi zaidi dun...