Posts

USIACHE KUONGEA NA WATU

Image
USIACHE KUONGEA NA WATU. Habari yako!  Ni matumaini yangu upo salama na unachukua tahadhari stahiki katika mapambano dhidi ya Korona. Unapojizuia kupata maambukizi pia wakumbushe wengine wajizuie. Usiache kuongea nao! Viumbe hai vyote vina njia za mawasiliano. Namna ya kuwasiliana kati yao hususani pale wanapotekea familia moja. Kwa mfano Simba kwa simba, Nyani kwa Nyani, Siafu kwa siafu nk. Wakati viumbe vingine vyote vinatumia milio ya asili zao na ishara kuwasiliana baina yao binadamu yeye anatumia Lugha yaani mpangilio wa sauti kuwasiliana. Binadamu anaongea. Katika kuongea kuna... ●Kuuliza  ●Kueleza/Kufafanua Katika maongezi yetu basi kuna mambo mawili tunayafanya nayo ni Kuuliza au Kueleza. Usiache kuuliza, usiache kueleza (kujieleza, kuelezea) vitu mbalimbali kwa watu waliokuzunguka. Watu wana vitu wanapitia, wana vitu wamezoea, wana vitu wanapenda jitahidi waongeleshe. Waulize ilikuwaje hivi? Wape nafasi wajieleze kuliko kuhukumu na kulaumu. Hakuna mtu mjin...

Watu wanaofaidika kupitia ujinga wako.

Image
"Baba shuleni wametuagiza kesho wanafunzi wote tuwe na Amoeba. Amoeba inauzwa 50000....." Naimani umewahi sikia kauli hizo kwenye stori au hata kuhusika kuwapiga hela wazazi na ndugu kwa kupitia kile wasichojua. Ujinga hauna faida ila kuna watu watanufaika na ujinga wako. Wahenga walikuwa sahihi sana waliposema "Wajinga Ndio Waliwao". Kupitia ujinga utaibiwa kizembe pasi matumizi ya silaha, utauziwa vitu kwa hati au risiti feki na baadae mambo yatageuka na utatapeliwa hutopata kile ulichonunua wala hela uliyonunulia haitorudi. Viongozi, wanasiasa na baadhi ya viongozi wa dini wa Kiafrika wanatujua sana. Wanajua wengi wetu ni wajinga. Hivyo hutumia ujinga wetu kunufaika katika kupata nyadhifa au kupata mali.  Atakuja kipindi cha kampeni atagawa pombe, vitenge, kofia na kutulisha pilau nyama tutahisi akipata uongozi hayo ndiyo yatakuwa maisha yetu ya kila siku na yeye ndiye mwarobaini wa matatizo yetu.  Kura zote kwake, akishinda uchagu...

Ujinga Utakufanya Uone Kila Kitu Kipo Sawa au Kila Kitu Kina Kasoro.

Image
Kuna madhara mengi sana ya ujinga. Ujinga huathiri hata mtizamo wa mtu na jinsi ya kuchukulia mambo. Ujinga humpofua mtu kiasi cha mtu kutoona mazuri au kutoona mabaya ndani ya kitu au jambo fulani. Mtu mjinga hujikuta haoni kasoro yoyote kwenye jambo yeye anaona kila kitu kipo sawa lakini pia anaweza asione zuri kwenye kitu fulani yeye anaona kila kitu kina makosa au kina kasoro. Ni vyema kutafuta au kujua ukweli wa jambo kabla ya kukosoa, kusifia au kuhukumu. Kwa mfano kwa kutokujua kanuni za kazi na maadili ya Uandishi wa habari mtu anaweza akamwona Mwandishi wa habari anapatia sana katika kazi yake ila kiukweli kuna dosari kadha wa kadha. Mtu mwingine naye kwa kutokujua anamwona mwandishi wa habari anakosea sana japokuwa kuna vitu vingi anapatia na ili ujue anapatia au kukosea na kwa kiwango kipi ni mpaka ujue kanuni za kazi yake, maadili na miongozo. Binti mmoja kwa jina la Ashura alikwenda kuishi kwa shangazi yake huko Muheza Tanga. Basi katika kuishi na k...

Njia 10 Nyepesi za kupata Maarifa Katika Mazingira ya Tanzania

Image
Maarifa ni taarifa iliyobeba ukweli, ufananuzi, ujuzi, uelewa wa jumla wa kitu fulani. Kuna njia mbalimbali za kutapa maarifa. Kwa mazingira yetu ya kitanzania kuna njia nyingi za kupata maarifa na zifuatazo ni njia 10 nyepesi za kutumia katika jamii zetu.... Njia 10 za kupata maarifa ● Kujisomea vitabu mbalimbali, magazeti, makala, Majarida, vitabu vya dini. Maarifa mengi yamewekwa kwenye mfumo wa maandishi. ●Kuhudhuria semina, vikao na warsha mbalimbali. Hiyo ni pamoja na ibada za dini, Kliniki za afya, maonyesho kama vile Nanenane na mikusanyiko mingine inayohusu utoaji wa elimu. ● Simulizi, maonyo, ushauri kutoka kwa wazee na watu waliotuzunguka . Dondoo za vitu na visa mbalimbali  vya kweli vya maisha hupatikana katika mfumo huu. Wazee wetu kwa uzoefu wao wa maisha na upendo wao kwetu hutuelimisha na kutupa mwongozo wa njia zipi salama katika mambo mbalimbali ya maisha. ● Kutazama Video zinazoelimisha (YouTube, Dokumentari, na vipindi vya k...

Ujinga ni kama Ugonjwa

Image
Ujinga ni kitendo cha kutokujua jambo au kitu fulani na kuathirika kwa kutokujua hilo jambo. Vivyo hivyo hata ugonjwa ni kuwa na vijidudu/vimelea mwilini na kuathirika kwa uwepo wa hivyo vimelea.  Kuna aina mbalimbali za magonjwa ila aina mbili kuu. Magonjwa ya kuambukizika na magonjwa yasiyoyakuambukizika. Ugonjwa wa kuambukizika mtu huupata kutoka kwa mwingine na kisha huuambukiza kwa wengine na mzunguzuko huendelea. Na ujinga upo katika mtindo huo. Mtu hupata maarifa asi kisha huyasambaza kwa wengine na kuwaaminisha na wale waaminio husambaza kwa wengine na wengine. Mwaka 2016 huko mkoani Dodoma wanakijiji wakishirikiana na uogonzi wa kijiji waliwaua kwa kuwachoma moto watafiti wa masuala ya ardhi. Moja ya watu wanaoheshimiwa na kuaminika pale kijijini alizusha kuwa wale wageni walioingia kwenye kile kijijini sio wataalamu kutoka kwenye taasisi bali ni wanyonya damu. Wanakijiji wakajazwa huu ujinga na wakijua wanyonya damu ni wauaji basi wakaona wawavamie...

Ujinga ni chanzo kikuu cha ubinafsi.

Image
Ubinafsi ni moja ya madhara ya ujinga. Mtu kuwa na hisia kali juu yake dhidi ya wengine. Kuona yeye ndio zaidi ya wengine kwenye hilo kundi, kuhisi anastahili kupata zaidi ya wengine mfano gawio la kitu chochote, kipato hata shukurani. Ubinafsi unaletwa na upofu wa uhalisia unaotokana na kutokujua uhalisia wa vitu au maisha na kujikuta unajiona au unajifikiria wewe tu  Ubinafsi ni ujinga. Kutokujua pia wenzako wana thamani kama wewe, ni wahitaji kama wewe, ni watafutaji kama wewe. Ubinafsi ni kutokujua kuwa ridhiki huja kwa baraka za Mungu, kwa jitihada na kwa uwekezaji lakini wewe unachojua ni unastahili zaidi yao hata kama mpo katika daraja moja au daraja la chini yao. Kutokana na ubora wako katika jambo fulani unaona HAKUNA KAMA WEWE!! Wakati kuna watu mnaosaidiana nao, wanaokupa mawazo na kukutia moyo. Au kuna watu ambao kama nao wangepewa nafasi kama wewe wangeweza kufanya kama wewe au hata zaidi. Kupuuzia michango ya watu wengine katika maf...

KUKATAA MAARIFA NI UJINGA ULIOKOMAA

Image
Naomba nianze kwa kucheka kidogo (haha ) kuna kauli nyingi sana zinazoumiza ukizisikia mtu akisema ila zinachekesha ukizitafakari. Bila shaka umewahi sikia kauli "Sikiliza wewe sisi ndio wataalamu....". Hiyo kauli ni moja ya kauli maarufu tu kwenye mitandao ya kijamii hapa nchini kwetu Tanzania. Nje ya hio kauli kuna kauli zingine kama.. ●Utaniambia nini wewe? ●We mtoto wa juzi unajua nini? ●We wakuja utatueleza nini sisi wazawa? ●Mkubwa hakosei ●Nimeanza kuliona jua kabla yako huna chakuniambia sikijui ●Kwani yenye elimu mkubwa wamenipita nini mimi?   Siwezi zitaja kauli zote kwakuwa ni nyingi na kila siku zinakuja kwa mfumo tofauti ila zote zinakuwa zimejengeka katika kukataa maarifa mapya au maarifa mbadala kutoka kwenye taasis za kutoa elimu au kutoka kwa watu waliotuzunguka.   Tangu kuumbwa kwa dunia mpaka leo hii nje ya mapungufu au kasoro zingine za kila mwanadamu, binadamu hajatimia kimaarifa. Kuna maarifa kila mwanadamu anakuwa na uhaba nayo au h...