Posts

Huduma ya Kangaroo Katika Malezi ya Mtoto

Image
Huduma ya Kangaroo katika malezi ya mtoto Mgusano wa ngozi kwa ngozi kati ya mzazi na mtoto maarufu kwa jina la  "Huduma ya Kangaroo" ni huduma ambayo wazazi hususani akina mama huwapa watoto wao kipindi wakiwa wachanga. Huduma hii inafaida kubwa kwa watoto na kwa wazazi pia, kwa kuwa inaongeza ukaribu kati yao. Huduma ya Kangaroo Maneno "huduma ya kangaroo" ilikuwa inaitwa kwa kufanana kwake na jinsi Kangaroo hubeba watoto wao. Huduma ya ngozi kwa ngozi huiga mazingira ya kinga na ya uleaji ya mfuko wa kangaroo. Kwa ufafanuzi, utunzaji wa kangaroo ni utunzaji wa maendeleo kwa kugusanisha ngozi ya watoto wachanga dhidi ya kifua cha mama au baba. Huduma ya kangaroo ilianza katika miaka ya 1970, kama njia ya kukuza utunzaji na kunyonyesha mapema kwa watoto wachanga wa waliozaliwa ndani wa muda. Mwishoni mwa 1970, shughuli hii ilipanuliwa kwa watoto wachanga waliozaliwa kabla ya miezi tisa kutokana na viwango vya vifo vingi, viwango vya juu vya maam...

HAKI ZA MGONJWA POPOTE PALE

Image
HAKI ZA MGONJWA Katika maisha kwa sababu  mbalimbali mwanadamu hupatwa na udhaifu wa mwili hivyo hujikuta akitafuta tiba kwenye taasisi za kutolea tiba za afya. Taasisi hizo hutoa huduma mbalimbali na katika kupokea huduma mgonjwa huwa na haki zifuatazo ● Haki ya kusikilizwa ●Mgonjwa ana haki ya kujua huduma za afya zinazotolewa katika hospitali, ikiwa ni pamoja na mkalimani endapo mgonjwa haimudu lugha ya kawaida katika eneo hilo. ●Haki ya kutaka gonjwa lake liwe siri ●Haki ya kuulizia na kuambiwa majibu ya vipimo vyake ●Haki ya kukataa kuendelea na matibabu ●Haki ya kuomba abadilishiwe mtalaamu (Daktari/Muuguzi) ● Mgonjwa ana haki ya kujua ni nani anayetoa huduma za matibabu na ni nani anayehusika na kumuhudumia.. ●Haki ya kupewa elimu ya kujikinga au kujiepusha na magonjwa ●Haki ya kupewa ufafanuzi toshelezi juu ya matumizi ya dawa ●Haki ya kupewa ufafanuzi wa gharama za matibabu yake ●Haki ya kuhudumiwa kama wagonjwa wengine bila ...

VIRUSI VYA KORONA KWA WAJAWAZITO NA WANAWAKE WANAONYONYESHA

Image
Ugonjwa wa Coronavirus (COVID-19) ni ugonjwa unaoambukiza unaosababishwa na virusi vya corona. Virusi hivi hushambulia mfumo na hewa na kuleta madhara kadha wa kadha kwenye mwili wa mwanadamu na hata kupelekea kifo.  Kumekuwa na nadharia na maswali mbalimbali juu ya virusi hivi kwa watoto wachanga, wajawazito na wanawake wanaonyonyesha juu ya namna ya uambukizaji na namna nzuri za kuzuia maambukizi. Hadi sasa hakuna utafiti unaothibitisha maambukizi ya COVID-19 kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto kupitia maziwa ya mama, maji maji katika mfuko wa uzazi (mtoto akiwa tumboni) au sampuli zingine kutoka kwa mama. Bado shirika la afya duniani linasema hakuna uthibitisho wa virus hai vya corona katika sampuli tajwa hapo juu. Lakini mpaka sasa kinachofahamika ni kwamba watoto kadhaa wamepatikana na virusi vya corona baada tu ya kuzaliwa na haijulikani kama walivipata wakiwa tumboni au baada ya kuzaliwa. Pia vipo visa vya mtoto wa miezi sita, miezi kumi na moja na visa ...

Kwanini virusi vya Uviko 19 vimekuwa hatari sana kwa wanaume kuliko wanawake?

Image
CORONAVIRUS KWA MWANADAMU NA WANAWAKE. Ulimwenguni kote - nchini Uchina, Italia, Marekani na Australia - wanaume wengi zaidi kuliko wanawake wanakufa kutokana na Uviko-19. Kwa nini? Je! Ni jeni, homoni, mfumo wa kinga - au tabia - ambayo inawafanya wanaume wanashambuliwa zaidi na ugonjwa? Ninaona kama mwingiliano wa mambo haya yote na sio tofauti na virusi vya SARS-Cov-2 - majibu tofauti ya wanaume na wanawake ni mfano wa magonjwa mengi katika mamalia wengi. Takwimu mbaya Huko Italia na Uchina vifo vya wanaume ni zaidi ya mara mbili ya ile ya wanawake. katika mji wa New York wanaume hufanya karibu asilimia 61 ya wagonjwa wanaokufa. Australia inaunda kuwa na matokeo sawa, ingawa hapa ni zaidi ya vikundi 70-79 na 80-89. Tofauti moja kuu katika ukali wa Uviko-19 ni umri. lakini hii haiwezi kuelezea upendeleo wa kijinsia unaonekana ulimwenguni kwa sababu kiwango cha kuongezeka kwa vifo vya wanaume ni sawa katika kila kikundi cha watu kutoka 30 hadi 90+. Wanawake pia...

NUTRITION, IMMUNITY AND CORONAVIRUS PANDEMIC

Image
NUTRITION, IMMUNITY AND CORONAVIRUS PANDEMIC I hope you are keeping safe and well during these challenging times.   During the coronavirus (COVID-19) pandemic where the whole world is affected, maintaining a healthy lifestyle is more important than ever. Due to the disruptions in the normal lifestyle of people, where most of the people spend most of the time in their homes, increasing the consumption of nutritious foods and doing physical activities to improve body immunity is very critical while we are fighting against this pandemic disease.   There are many emerging myths and misconceptions about food and nutrition in Tanzania and other parts of the world during coronavirus (COVID-19) pandemic. It should be noted that, myth or misconception can be damaging especially during this critical time of coronavirus pandemic and therefore we should only focus on nutrition facts as recommended by health professionals.  Some of the nutrition myths/misconcepti...

USIACHE KUONGEA NA WATU

Image
USIACHE KUONGEA NA WATU. Habari yako!  Ni matumaini yangu upo salama na unachukua tahadhari stahiki katika mapambano dhidi ya Korona. Unapojizuia kupata maambukizi pia wakumbushe wengine wajizuie. Usiache kuongea nao! Viumbe hai vyote vina njia za mawasiliano. Namna ya kuwasiliana kati yao hususani pale wanapotekea familia moja. Kwa mfano Simba kwa simba, Nyani kwa Nyani, Siafu kwa siafu nk. Wakati viumbe vingine vyote vinatumia milio ya asili zao na ishara kuwasiliana baina yao binadamu yeye anatumia Lugha yaani mpangilio wa sauti kuwasiliana. Binadamu anaongea. Katika kuongea kuna... ●Kuuliza  ●Kueleza/Kufafanua Katika maongezi yetu basi kuna mambo mawili tunayafanya nayo ni Kuuliza au Kueleza. Usiache kuuliza, usiache kueleza (kujieleza, kuelezea) vitu mbalimbali kwa watu waliokuzunguka. Watu wana vitu wanapitia, wana vitu wamezoea, wana vitu wanapenda jitahidi waongeleshe. Waulize ilikuwaje hivi? Wape nafasi wajieleze kuliko kuhukumu na kulaumu. Hakuna mtu mjin...

Watu wanaofaidika kupitia ujinga wako.

Image
"Baba shuleni wametuagiza kesho wanafunzi wote tuwe na Amoeba. Amoeba inauzwa 50000....." Naimani umewahi sikia kauli hizo kwenye stori au hata kuhusika kuwapiga hela wazazi na ndugu kwa kupitia kile wasichojua. Ujinga hauna faida ila kuna watu watanufaika na ujinga wako. Wahenga walikuwa sahihi sana waliposema "Wajinga Ndio Waliwao". Kupitia ujinga utaibiwa kizembe pasi matumizi ya silaha, utauziwa vitu kwa hati au risiti feki na baadae mambo yatageuka na utatapeliwa hutopata kile ulichonunua wala hela uliyonunulia haitorudi. Viongozi, wanasiasa na baadhi ya viongozi wa dini wa Kiafrika wanatujua sana. Wanajua wengi wetu ni wajinga. Hivyo hutumia ujinga wetu kunufaika katika kupata nyadhifa au kupata mali.  Atakuja kipindi cha kampeni atagawa pombe, vitenge, kofia na kutulisha pilau nyama tutahisi akipata uongozi hayo ndiyo yatakuwa maisha yetu ya kila siku na yeye ndiye mwarobaini wa matatizo yetu.  Kura zote kwake, akishinda uchagu...