Posts

Showing posts from 2020

Shairi: IWAJE?

Image
IWAJE? Wewe ulitakaje? Shule za msingi Vitu vifanyikaje? Katikati ya vipindi Watoto walaje? Kwa elimu-ushindi Mimi kama wewe Nina uwezo kufikiri Nafikiri mwenyewe Siwezi shikiwa akili Mwenye haki apewe Vinginevyo ni ukatili Haki ya kuelimika Na malezi stahiki Hakizo kuzishika Mtoto huwa rafiki Mzaziye wajibika Utajaona mantiki Mapumziko wasile! Darasani waingie Njaa iwazingile Somo lisiwaingie Shule waikimbie Maoniyo niambie? Wale chakula vizuri Darasa changamfu Wasipate tena sifuri Utoro ugeuke hafifu Wawe watoto wazuri Wenye afya nadhifu. Changia mawazo Tupate mwongozo Tuwajengee uwezo Elimu bora ni nguzo Hatua hizi mwanzo Tuvishinde vikwazo #NilisheNifaulu Fasmo Tanzania Nobel was Here😊

NILISHE NIFAULU

Image
NILISHE NIFAULU Ni mradi unaotekelezwa na asasi isiyokuwa ya kiserikali ya FASMO ikishirikiana na wanajamii. Mradi huu umelenga utoaji wa chakula katika shule za msingi kama njia kuu ya kuchochea mahudhurio na utulivu wakati wa kujifunza ambavyo kwa pamoja huchangia matokeo bora (ufaulu) kwa wanafunzi na shule kwa ujumla. Familia nyingi za Kitanzania zina uwezo mdogo wa kiuchumi. Watoto hulazimika kuamka asubuhi sana na kukimbilia shule bila kupata kitu chochote cha kula. Na kwa bahati mbaya hata shuleni hakuna utaratibu wa ugawaji wa chakula hivyo mtoto hujikuta masaa zaidi ya saba hajapata chakula kwa kuwa hata hela ya matumizi shuleni hajapewa au ni ndogo sana.  Uelewa wa wanafunzi huwa hafifu kutokana na mazingira hayo ya ukosefu wa chakula wakati wa masomo. Pia ukosefu wa chakula huchochea sana utoro na wanafunzi kuacha shule.  Utoro katika sura mbili, sura ya kwanza wanafunzi kutokuja shule na sura ya pili mwanafunzi au wanafunzi kutohudhuria kipindi au vi...

SIKU YA CHAKULA DUNIANI

Image
Tarehe 16 mwezi oktoba kila mwaka ni maadhimisho ya Siku ya chakula duniani. Siku hii ilihasisiwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Kilimo na Chakula, (FAO) mnamo mwaka 1979. Tarehe ya leo pia ni maadhimisho ya miaka 75 ya FAO tangu kuanzishwa kwake. Lengo kuu la maadhimisho haya ni kuongeza uelewa kwa watu kuhusu umuhimu wa chakula na uhakika wa chakula na lishe kwa watu wote duniani hasa wale walio katika hatari ya kukosa chakula kabisa. Chakula ni moja kati ya mahitaji muhimu ya kila binadamu, hivyo ni sehemu ya maisha yetu kila siku kwa kuwa bila chakula uhai wetu hutetereka. Hivyo, tunaposherehekea siku ya chakula duniani, jiulize; 1. Nina uhakika wa chakula? Kama ndiyo (naweza kununua, kuandaa na kula chakula cha kutosha) je vipi kuhusu ambao hawawezi kula hata mlo mmoja kwa siku? 2. Chakula ninachokula ni salama? Ni kisafi, kimeandaliwa katika hali gani, hakina vijidudu vyovyote au sumu ya aina yoyote itokanayo na vijidudu hivyo (kama vile sumukuvu itokanayo na kuvu ...

HAKI ZA AFYA YA UZAZI NA JINSIA

Image
HAKI ZA BINADAMU Haki za binadamu ni haki zinazohusiana na mambo ya msingi na asili ya uhuru na heshima ya ubinadamu ambapo watu wote wamepewa haki ya kupata heshima kama binadamu. Mara mtu azaliwapo mume au mke hupata haki hizi. Haki hizi zinatambuliwa kimataifa na zina usawa kwa watu wote. Nchi mbalimbali zimetia sahini na kuidhinisha haki hizi za kimataifa na kufanya ni sehemu ya sheria zao pamoja na kuweka sera zinazolinda haki hizi. HAKI ZA UZAZI Haki za uzazi ni haki zinazomwezesha mwanamke na mwanaume, mwajiriwa kutimiza majukumu yake ya uzazi na kufanya kazi bila kubaguliwa, kubugudhiwa au kupoteza ajira. Likizo ya uzazi ikiwa ni moja ya haki za uzazi, humpa mama na baba muda kutoa matunzo muhimu kwa mtoto katika siku/miezi ya mwanzo ya maisha yake, ikiwa ni pamoja na kumnyonyesha. Vilevile likizo ya uzazi humpa mama mwajiriwa muda wa kupumzika na hivyo kusaidia mwili wake kurudi katika afya na hali ya kawaida baada ya kujifungua. Haki za uzazi zina misi...

Shairi: BINTI MTOTO WA KIKE

Image
Poem Leo ndio ile siku yao, Mabinti kusherekea, Waongee vitu vyao, Yatupasa vipokea, Magumu waseme wao, Yawapasa kuendelea. Binti Mtoto wa kike,  Amka kwa pambazuka, Yenye tija uyashike, Wakati wako umefika, Kimaendeleo utumike Wasiokuamini kuaibika. Punguza kupiga soga, Na umbea kila kukicha,  Wahabarishe mashoga, Waamke kumekucha, Waachane na uoga, Maendeleo kujiepusha Kujituma iwe tabia, Usingoje uhimizwe, Jamii inakusubiria, Ndoto zako utimize, Yasokufaa kimbia, Usisubiri yakuumize. Mimba kabla ya ndoa, Rafiki hilo usithubutu, Kimaisha litakupopoa, Na kushusha wako utu, Haswa akikataa kukuoa, Ndoto zako tapata kutu. Wewe mtu adhimu, Acha leo nikupashe, Ndoto zako muhimu, Usikubali usiziache, Ongeza na nidhamu, Sibwetekee uchache. AMIN Na  Nobel Edson  Fasmo Tanzania 0783961492

Siku ya Wazee Duniani

Image
Ukiwa ni mwanzo kabisa wa mwezi wa kumi baada ya kumaliza miezi tisa ya mwaka 2020 iliyojaa mikasa mingi ya kusisimua kwenye nyanja mbalimbali za maisha hususani afya na uchumi.  Leo ni tarehe mosi ya mwezi Octoba na ni Siku ya Wazee Duniani.   JE WAJUA  ❗️Kila sekunde mbili inayopita watu wawili duniani wanatimiza miaka 60? .  Mzee ni mtu mwenye busara nyingi, mlezi wa jamii na amebeba mafundisho mengi kwa kuwa ameona n kujifunza mengi katika Maisha.   Kutokana na majukumu wanayoyapitia wazee, huweza kukumbana na matatizo ya kiafya kama vile kusumbuliwa na magonjwaa kwa mfano shinikizo la juu la damu, kisukari, na maumivu ya viungo vya mwili kama vile miguu, mgongo na misuli. Pamoja na hayo, wazee husumbuliwa na; *Msongo wa mawazo ambao mara nyingi husababishwa na kuwekwa mbali na wanafamilia, kukosa wazee wenzake wakabadilishana mawazo. *Kukosa kipato toshelezi kuzimudu gharama za maisha na matibabu. Katika kuadhimisha siku ya wazee dunia na  ...

MAADHIMISHO YA SIKU YA MOYO DUNIANI

Image
Siku ya moyo duniani huadhimishwa tarehe 29 mwezi septemba kila mwaka. Shirikisho la moyo duniani ndio chimbuko la siku hii muhimu yenye lengo la kusaidia jamii kujua madhara ya magonjwa ya mfumo wa mzunguko wa damu ambapo zaidi ya nusu ya vifo vyote vitokanavyo na magonjwa yasiyo ya kuambukiza duniani husababishwa na magonjwa haya.  Hapo awali siku ya moyo duniani ilikuwa ikiadhimishwa jumapili ya mwisho ya mwezi wa tisa na kwa mara ya kwanza iliadhimishwa tarehe 24 septemba 2000. Magonjwa ya mzunguko wa damu husababisha takribani vifo vya watu milioni 17.9 dunia nzima na vifo hivi haswa huhusisha magonjwa ya moyo na kiharusi (stroke). Hii huchangia takribani asilimia 31 ya vifo vyote duniani. Moyo ni ogani ifanyayo kazi kama pampu inayosukuma damu kupitia mirija katika mwili wa binadamu na hivyo husaidia katika kusafirisha na kuzungusha virutubishi na hewa za oksijeni, kabonidayoksaidi pamoja na vitu vingine vingi. Moyo huanza kufanya kazi kuanzia siku ya 22 tangia kutung...

UMUHIMU WA KUSOMA MABANDIKO YA LISHE KWA MLAJI

Image
UMUHIMU WA KUSOMA MABANDIKO YA LISHE KWA MLAJI                                                 Mabandiko ya lishe ni maandishi yanayompatia mlaji taarifa mbalimbali juu ya bidhaa na thamani ya lishe inayo patikana kwenye chakula ambacho anataka kununua, mabandiko ya lishe huwa yanaandikwa haswa kwenye vyakula ambavyo vipo katika vifungashio mbalimbali kama vile chupa za maji, mifuko ya maziwa na juisi. Taarifa zinazowekwa kwenye mabandiko ni pamoja na kiasi cha kutumika  ,idadi ya kalori, kiasi cha mafuta, virutubishi vinavyo patikana pamoja, ujazo wa chakula, muda wa matumizi, kanuni za matumizi na viungo viivyotumika katika kutengeneza chakula husika. Shirika la Viwango Tanzania (TBS) ni shirika ya kiserikali ambalo linasimamia ubora, usalama wa chakula kwa mlaji. Kila bidhaa ya chakula kabla haijaingia sokoni na kumfikia mlaji ni lazima kwanza ihakikiwe ubora wake kwa matumizi, jinsi ilivyo tengenezwa, usalama wake na kisha kubandikwa mabandiko ya lishe ili kumsaidia mla...

FAIDA ZA MAZIWA YA MAMA KWA MTOTO

Image
FAIDA ZA MAZIWA YA MAMA KWA MTOTO Maziwa ya matiti ni maziwa yanayotolewa na mama ili kumnyonyesha mwanawe. Maziwa hayo hutoa chanzo msingi cha lishe kwa watoto kabla ya wao kupata uwezo wa kula vyakula vingine, yaani watoto wachanga hadi umri kadri wanavyoweza kuendelea kunyonyeshwa.  Kunyonyesha ni tendo la kumpa mtoto maziwa kutoka katika titi la mama moja kwa moja au kumnywesha mtoto maziwa ya mama yakikamuliwa kwa kutumia kikombe.  Maziwa ya mama ndiyo chakula bora kwa mtoto mchanga kuliko maziwa wengine au chakula kingine. Shirika la Afya duniani (WHO) linapendekeza mtoto kunyonyesha maziwa ya mama pekee kwa miezi sita ya kwanza ya maisha, vyakula vizito huanzishwa mnamo umri  huu unapoongezeka,  hatua kwa hatua wakati ishara ya utayari huonekana, kunyonyesha huendelea kupendekezwa kama nyongeza mpaka angalau miaka miwili, au kwa muda mrefu jinsi mama na mtoto watakavyotaka. Maziwa ya mama ni chakula na kinywaji cha kwanza, na cha pekee kwa mtoto tangu anapozaliwa mpa...

SIKU YA KUPINGA WATU KUJIUA DUNIANI.

Image
Wanaojiua wote ni wajinga? Kujiua ni kuandamwa na roho mbaya ya mauti? Kujiua ni kujiadhibu tu? Kujiua ni kufanya maamuzi kwa kukurupu.... Kujiua ni kufika mwisho wa kufikiri... Kila mmoja anaongea lake juu ya anachokiona ni sawa pale anaposikia mtu kajiua. Bila kujali fikra zote hizo, ukweli ni kwamba watu wanajiua sana.  Kwa takrimu kwa kila sekunde 40 mtu mmoja hujiua duniani. Ukipiga mahesabu hapo kwa harakaharaka kwa wiki watu 630 hujiua duniani. Chanzo ni nini? Wapo wanaojiua na kuacha ujumbe wa sababu za kwanini wametoa uhai wao, na wapo ambao hujiondoa tu bila kuacha ujumbe wowote juu ya nini kimepelekea maamuzi yake hayo. Wote kwa pamoja huacha simanzi kubwa kwa wapendwa wao. Sababu ya ugumu wa maisha, sababu ya matatizo ya akili, sababu ya magonjwa sugu, sababu ya msongo wa mawazo usiohimilika kama vile aibu baada ya kufanyiwa tendo baya, sababu ya mapenzi, sababu ya ugaidi na kisasi ni sababu maarufu kati ya sababu nyingi zinazopelekea watu kujiny...

Msingi Wa Lishe Bora katika shule mbalimbali

Image
Mapema leo timu zetu ya Wataalamu wa lishe tulitembelea shule ya msingi Mwembesongo, Bungo na Mchikichini B zilizopo Morogoro mjini. Dhumuni kubwa la matembezi haya ni kutoa elimu na kukumbushana na wanafunzi pamoja na waalimu wao juu ya ulaji bora huku tukilenga zaidi kuhamasisha ulaji wa mboga za majani, samaki na maziwa ambavyo vinafaida lukuki mwilini. Kwa mwanafunzi ni ngumu kula anavyotaka kwa kuwa kula kwake kuna tegemea wazazi, lakini akianzwa kujengwa kiakili juu ya ulaji wa afya pasi na shaka kadri anavyokua mkubwa ataishi ile elimu na kuwa na afya njema kwa kuwa atakuwa anakula vizuri kadri ya mahitaji ya mwili. Wahenga wanasema SAMAKI MKUNJE ANGALI MBICHI akikauka ni ngumu sana kukunjika.  Wanafunzi wa shule zote zilizotembelewa na wataalamu wa Lishe wamekuwa wachangamfu na wasikivu wakati wa upataji wa elimu. Hii imechochea uelewa wao kuwa mzuri na kuzidi kuhamasika na ulaji wa afya.  Tutazidi kutembelea shule nyingine zaidi hapa mjini M...