Posts

Showing posts from June, 2020

RUSHWA YA NGONO KATIKA MAPANA YAKE.

Image
RUSHWA YA NGONO KATIKA MAPANA YAKE. Rushwa ya ngono ni moja ya rushwa maarufu na ya kawaida kuombwa na hata kutolewa katika jamii zetu. Aina hii ya rushwa ina mizizi sana kwenye taasisi mbalimbali hususani maeneo ya kazi, biashara na vyuoni. Rushwa ni kitu chochote kinachoombwa au kinachotolewa visivyohalali ili mtu apate kitu fulani ambacho kinaweza kuwa haki yake au sio haki yake. Kuna aina na mitindo mbalimbali ya rushwa katika jamii za maisha ya mwanadamu. Kati ya hizo aina mbalimbali, rushwa ya ngono ni moja wapo. Kama zilivyo rushwa zingine kutolewa katika uficho, rushwa ya ngono hufanyika katika usiri mkubwa sana baina ya hao watu wawili. Waathirika wakubwa wa hii rushwa ni wanawake. Inakuwaje? Kuna mazingira mbalimbali yanayopelekea rushwa ya ngono kuombwa na kutolewa. Kwa mfano rushwa ya ngono vyuoni ina sura kama tatu..  1. Kuna ile hali binti yupo vizuri kimasomo ila mhadhiri anamuwekea mizengwe na kutishia kumfelisha asipolala nae. 2. Kuna ile hali binti hayuko ...

SHAIRI: NJIA PANDA

Image
NJIA PANDA Nipo njia panda, Mawazo yanizonga, Kiza kimetanda, Fikra zanigonga, Wapi pa kwenda, Kivipi nitasonga? Niache shule, Nikatumie kipaji, Niwe kama yule, Msanii mchezaji, Nivume huku kule, Kwa mdogo mtaji. Nitakuwa maarufu, Na hela kibao, Sitaishi kwa hofu, Yatakuwaje mafao, Hawatoacha kunisifu, Katika maongezi yao. Nitajenga majumba, Nakumiliki magari, Kupitia kuimba, Nitakuwa hodari, Kwa udi uvumba, Nitaiteka sayari. Shule kitu nyeti, Lakini mimi sielewi, Kwanini wenye vyeti, Nafasi hawapewi, Kwenye viti waketi, Haki hawatendewi. Shule haina manufaa, Wasomi maisha duni, Sasa wanatuhadaa, Kisiasa kuturubuni, Kutuaminisha wanafaa, Wajinufaishe kiuchumi. Kipaji changamoto, Nani wa kukusaidia, Utaishia kwenye msoto, Na kuchoka kuvumilia, Utalia kama mtoto, Ndoto zisipotimia. Elimu bado hazina, Kote ulimwenguni, Kuiacha hapana, Hata wakinirubuni, Nitakosa maana, Wataniita muhuni. Shairi la watoto..... Na Nobel Edson Sichaleh Fasmo Tanzania  Childhood Develop...

SIKU YA SICKLE CELL DUNIANI

Image
Tarehe 19 juni ni siku inayotambulika na Umoja Wa Mataifa kama siku ya selimundu duniani ambayo lengo lake ni kuhamasisha watu kitaifa na kimatataifa kutambua uwepo wa aina hii ya ugonjwa unaotokana na mapungufu ya kijenetiki. Umoja Wa Mataifa unatambua ugonjwa huu kama moja ya magonjwa ya kijenetiki unaowakumba sana watu na ni tatizo kubwa linaloathiri watu wengi katika jamii zetu. Kwa kawaida seli nyekundu za damu huwa na muonekano wa duara unaoziruhusu kufanya shughuli zake kiurahisi na kwa ufanisi mwilini. Selimundu (sickle cell disorders) huhusisha magonjwa yote ambayo huathiri seli nyekundu za damu na kuzifanya kuwa na muonekano wa mundu 🌙 (muonekano wa kikwakwa kama cha kukatia nyasi) na ugonjwa huu ni wa kurithi kwa maana kwamba mtu huupata kutoka kwa wazazi wake na hauwezi kuambukizwa kutoka kwa watu wengine tofauti na wazazi wa mtu husika.  Tafiti zinaonesha Tanzania ni moja kati ya nchi duniani ambazo kuna watoto wengi huzaliwa na magonjwa ya selimun...

BABA KAMA BABA

Image
Baba la Baba Leo tarehe 21 June ndiyo siku ya wenye miji, watu wenye maamuzi nyumbani, watu wenye sauti popote pale ndani hata nje ya nyumba. Ni ukweli, leo ni siku ya watu ambao hawaoni shida kuvuja jasho ili wengine wafurahie leo na kesho yao. Kwa uthabiti kabisa na kuiweka familia nzima mabegani na kutembea huku kaibeba bila kujali hali ya nchi kiuchumi au iwe mvua liwe jua majukumu yake lazima atekeleze. Leo ni siku ya akina Baba Duniani, watu wenye mioyo yao. Kwa muda sasa kumekuwepo kwa siku hii adhimu ya kuhadhimisha uwepo wa akina Baba na mchango wao katika maisha na ustawi wa wanafamilia. Baba ni mzazi wa kiume, baba ni kiongozi wa familia (kwa mila za sehemu nyingi duniani).  Kutokana na tamaduni na hali ya maisha ya Afrika akina baba ndiyo wamekuwa watafutaji wakubwa wa mkate wa kila siku katika familia. Kipato hicho ndiyo kitagawanywa na kutumika kama chakula, kama ada, manunuzi ya nguo za wanafamilia, nauli za hapa na pale na matumizi mengine mengi yasiyo na id...

MTOTO WA AFRIKA

Image
Mwaka1991, wakuu wa nchi wanachama wa OAU walianzisha Siku ya Mtoto wa Afrika (DAC) kama kumbukumbu ya uasi dhidi ya wanafunzi 16 Juni 1976 huko Soweto, Afrika Kusini. Wakati huo, wanafunzi watoto wadogo waliandamana, mosi kupinga aina ya elimu duni ya kibaguzi waliyopewa na serikali ya kibeberu, pili waliitaka serikali ya mzungu iwape ruksa kufundishwa kwa lugha zao wenyewe.  Siku ya Mtoto wa Afrika hutumika kuwakumbusha watoto wetu hatua ya kijasiri waliyoichukua wenzao huko Afrika Kusini katika kulinda haki zao. Watoto wanakumbushwa kwamba wanaweza kuleta mabadiliko hata wakiwa wadogo Katika kuadhimisha siku ya mtoto wa Afrika ni vyema kukumbuka mambo kadhaa ili kufanikisha kuijenga Afrika imara kupitia watoto; 1. Tuishi na watoto kama marafiki zetu Katika maisha ya kila siku ni vyema kuishi na watoto kama marafiki zetu wa karibu sana bila kusahau majukumu yetu kama wazazi au walezi wao. Upande mzuri wa kufanya hivi ni kuongeza ukaribu na watoto ambao kwa tamaduni za...

MAISHA YETU YA KILA SIKU NA UCHANGIA WA DAMU.

Image
Juni 14 ni siku ya kuadhimisha kuchangia damu duniani. Siku hii hutumika kuwashukuru watu wote wanaojitolea kuchangia damu na kuhamasisha wengine ili waweze kuanza kuchangia damu. Damu hutumika kusaidia kuokoa maisha ya watu wengi sana duniani kama vile, watu waliopata ajali, wanawake wanaojifungua na watu wenye magonjwa mbalimbali kama vile upungufu wa damu mwilini (anemia). Kuchangia damu ni kitendo cha mtu kutoa damu yake ambapo huhifadhiwa katika mfuko maalum (blood bag) na kuwekwa katika joto kati ya nyuzi joto (°c) +2 hadi +6. Joto hilo ni sahihi katika kuhakikisha vitu vilivyomo ndani ya damu kama vile seli nyekundu, chembe sahani na vinginevyo haviharibiwi na damu haishambuliwi na vijidudu hatari kama vile bakteria na virusi. Tujikumbushe vitu vichache kuhusu damu na kuchangia damu Damu ni moja kati ya tishu katika miili ya wanyama (binadamu) ambayo hutumika kusafirisha virutubishi, takamwili, oksijeni, homoni na vitu vingine mwilini..Uwepo wa seli nyekundu za damu ...

SIKU YA WATU WENYE UALBINO DUNIANI.

Image
Siku ya watu wenye ualbino duniani Ualbino ni hali ambayo husababishwa na kurithi jeni (genes) kutoka kwa wazazi wote wawili ambapo mtoto hukosa melanini (rangi ya asili-pigmentation). Rangi ya asili hukosekana katika macho, ngozi, nywele na kupelekea kuwa na uoni hafifu na kuwa katika hatari ya kupata saratani ya ngozi. Ikumbukwe kwamba wazazi wote wanaweza wasiwe na ualbino lakini kama walibeba jeni za ualbino, hii ndio hupelekea wao kupata mtoto mwenye ualbino kwa maana kwamba wao walibeba tu zile jeni ila hazikuoneshwa katika maumbile. Barani Afrika Tafiti zinaonesha kuwa idadi ya watu wanaoathirika na ualbino ni kubwa kusini mwa jangwa la sahara ambapo kwa Tanzania inakadiliwa mtu 1 kati ya 1400 ana ualbino, kwa utafiti uliofanyika nchini zimbabwe ulionesha mtu mmoja kati ya 1000 ana ualbino. Ni vyema kukumbuka pia ualbino hutokea kwa viumbe wengine kama vile mbwa, simba, tembo, taiga na wanyama wengine wengi. Baadhi ya changamoto ambazo watu we...

USALAMA WA CHAKULA NI SUALA LA KILA MTU

Image
Mpendwa msomaji wa makala zetu, tunayofuraha kukukaribisha tena kwenye blog yetu siku ya leo tarehe 7 Juni ambayo pia ni siku ya kuhadhimisha Usalama wa Chakula Duniani. Chakula ni kitu chochote kinachoweza kuliwa na kuupatia mwili virutubishi na kinakubalika kijamii. Tunaposema kukubalika kijamii ni kama vile panya anakubalika kama chakula kule Mtwara lakini sio Chakula Mbeya kwakuwa jamii ya watu wa Mbeya haikubali ulaji wa panya.  Kuna vyakula aina mbalimbali lakini vyote vimegawanywa katika makundi matano kutokana na mfumo na kazi ya chakula mwilini. Usalama wa chakula ni kutokuwepo kwa hatari au viwango vinavyokubalika vya hatari katika chakula ambayo inaweza kuumiza afya ya watumiaji. Hatari inayosababishwa na chakula inaweza kuwa ya kimelea, ya kemikali au ya asili na kawaida haonekani kwa jicho wazi: bakteria, virusi, au mabaki ya wadudu ni baadhi ya mifano . Usalama wa chakula ni jukumu muhimu katika kuhakikisha kuwa chakula kinakaa salama katika kila h...

MAZINGIRA NA DUNIA YETU

Image
Mazingira ni wewe na mimi, mawe, miti, anga wanyama na kila kitu tunachokiona na tusichokiona kama vile vijidudu ambavyo vinaweza kuonekana kwa msaada wa vifaa maalumu vya maabara. Mazingira ndio chanzo cha hali ya hewa, chakula, hewa tunayoivuta (oksijeni), maji tunayokunywa na vitu vingine kede kede vyenye manufaa kwetu.. Vitu vyote katika mazingira hutegemeana. Kwa namna kwamba viumbe hai hutegemea viumbe hai wengine na visivyo hai ili maisha yaende. Kwa namna hii kunakuwa na matumizi ya vitu katika mazingira kwa namna fulani ambayo inaweza ikawa inafaa au ikawa isiyofaa. Kwa mfano binadamu hutumia mimea (miti) kama kuni au kutengeneza mkaa kwa ajili ya nishati ya kutumia majumbani na sehemu zingine, lakini tumeshafika mahali ambapo matumizi ya miti kwa ajili ya shughuli kama hizi na nyingine nyingi yamepelekea kuharibika na kupotea kwa uoto asili na kupelekea madhara katika hali ya hewa, mfano kuongezeka kwa jotoridi na kupungua kwa kiasi cha mvua duniani..  ...

MAZIWA KAMA MAZIWA (Shairi)

Image
MAZIWA KAMA MAZIWA Maziwa yamejaa lishe, Kuchochea afya nzuri, Ngoja leo nikuelimishe, Hili jambo la maakuli, Faida nizibainishe, Unywaji uwe vizuri. Kinywaji burudishi, Hakika afya chafaa, Kimejaa virutubishi, Na madini kadhaa, Kiweke kwenye pishi, Chakula kitamu balaa. Kimejaa protini, Wanga jitosheleza, Utashiba vitamini, Maji mwilini utaongeza, Mafuta na madini, Maziwa sio yakubeza. Mifupa huimarika, Kinga huongezeka, Hutoweza kutaabika, Mbeleni ukizeeka, Yafaa kwa kila rika, Na mwili hutosheka Ya ng'ombe au mbuzi, Kunywa kila mida, Wanashauri wajuzi, Mwilini hutopata shida, Changanya na mchuzi,  Mwili upate faida. Mwambie na jirani, Elimu hii imfikie, Maziwa si utani, Kunywa asipuuzie, Akisema ni uzamani, Faida zake msisitizie. Na  Nobel Edson Sichaleh, Fsmo Tanzania. Nutritionist and Consumer Scientist 0783961492

MAADHIMISHO YA SIKU YA MAZIWA DUNIANI

Image
Siku ya Maziwa Duniani huadhimishwa kila mwaka mnamo Juni 1. Siku hiyo ilianzishwa kwanza na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa ili kuonyesha umuhimu wa maziwa duniani. Imekuwa miaka 20 tangu maadhimisho yaasisiwe. Leo, ulimwengu mzima unasherehekea siku hii ili kuashiria umuhimu wa matumizi ya maziwa katika lishe yetu . Kwa kutimiza miaka ishirini maadhimisho ya mwaka huu yamebeba ujumbe wa "MAADHIMISHO YA MIAKA 20 YA SIKU YA MAZIWA DUNIANI."  Leo ni kilele cha wiki ya maziwa, tangu tarehe 26 Mei,, Jukwaa la Maziwa la Ulimwenguni na idara mbalimbali za maziwa za nchi nyingi duniani zimekuwa zikiadhimisha kwa kufanya mikutano na wadau na washiriki kuzungumza juu ya faida za maziwa na kuwatia moyo wengine kujumuika nao, pamoja na kuangazia shida za kupata maziwa na bidhaa za maziwa katika sehemu kadhaa za ulimwengu. Unywaji wa maziwa nchini kwetu Tanzania bado upo chini. Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) yampasa mtu mmoja kunywa ...